Header Ads Widget

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DK. MWIGULU NCHEMBA ASEMA HAWANA NIA YA KUZICHUKUA FEDHA ZA ASASI ZA KIRAIA

Siku moja baada ya kuibuka mjadala mkali kutokana na kauli aliyoitoa, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali haina nia ya kuchukua fedha za Asasi za Kiraia (Azaki) kutoka kwa nchi wa hisani ila ufadhili huo unapaswa kuendana na malengo ya nchi.

Mwigulu ametumia ukurasa wake wa Twitter kutoa ufafanuzi huo kama alivyofanya juzi alipotoa kauli iliyoibua utata na kupokelewa kwa hisia tofauti na wana Azaki.

Kauli yake ilisomeka, “Leo kupitia kikao tulichofanya kwa njia ya mtandao, nimeliomba Shirika la USAID kuelekeza kiasi cha msaada wa Sh3 trilioni inazotaka kuipatia Tanzania kupitia asasi za kiraia, zielekezwe kwenye miradi ya kimkakati ya Serikali ya Awamu ya Sita. Tutazisimamia vizuri,”.

Kauli hiyo ilionekana kuwashutua viongozi wa asasi za kiraia akiwemo Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa aliyeeleza kwa kuwa kazi zinazofanywa na asasi za kiraia hazitoki nje ya mipango ya Serikali na asasi zinawafikia wananchi kwa ukaribu zaidi.

“Alichotakiwa kufanya waziri ni kusisitiza asasi za kiraia kufanya kazi zake kwa kufuata hiyo miradi ya Serikali, lakini si kuzuia fedha zisielekezwe upande huo, asasi zina umuhimu wake na zinahitaji fedha ili zijiendeshe na kuwafikia kwa ukaribu zaidi wananchi kupitia miradi,” alisema Olengurumwa.
 
IENDELEA KUSOMA HAPA👇
 
SOMA HAPA ZAIDI ; CHANZO MWANANCHI.

Post a Comment

0 Comments