Header Ads Widget

DAYCARE CENTRE 71 ZAFUNGIWA MANISPAA YA KAHAMA

 

Na kareny Masasy


JUMLA   ya vituo 71 vya kulelea watoto mchana  (day care center) katika halmashauri ya manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga vimefungwa kutokana na kukiuka utaratibu na muongozo uliopo na badala yake wamiliki wake wamegeuza kuwa  shule zisizo rasmi na kuanza kufundisha. 

 Ofisa ustawi wa jamii  manispaa hiyo Abrahaman  Kibagaya amesema hayo jana  katika  zoezi linalo endelea la kukagua vituo  vya kulelea watoto Kama vimezingatia   muongozo ikiwemo programu jumuishi  ya kitaifa ya malezi  na makuzi ya maendeleo ya awali ya mtoto (PJT MMMAM) ambapo alisema kuwa Kati ya vituo 98  vilivyopo vituo sita tu ndiyo vyenye usajili wa kulea watoto mchana.

Kibagaya  alisema kuwa jumla ya vituo  71 vya kulelea watoto mchana vimefungiwa kwa kukosa sifa na vituo 21 vimepewa muda wa kusajili kwa kuonekana kidogo wameweza kukidhi matakwa ya muongozo kwa kuwa na walezi wenye sifa na eneo la michezo na darasa lenye dhana za ujifunzaji wa awali kwa mtoto.

 "Vituo 92 vimebainika kutokuwa na usajili na kuviendesha kinyemela bila kufuata utaratibu na muongozo unaotakiwa kwa maana ya kulea watoto wenye umri  wa kuanzia miaka miwili  hadi minne  na sio kuandika Kama wanavyofanya sasa  inatakiwa  kuwawekea dhana za ujifunzaji,michezo na kuimba pekee"alisema  Kibagaya

Kibagaya  alisema kuwa wazazi wamekuwa wakiibiwa fedha zao kwa kutoelezwa ukweli na wamiliki wa vituo wanapowapeleka watoto kulelewa  ni wajue ni mbadala wa dada wa kazi kwanza wanawachanganya wenye umri wa miaka miwili na minne  darasa moja na kuanza kuwafundisha kuandika na kupewa kazi ya kuandika awapo nyumbani (homework).

"Nimewaomba wenye vituo ambavyo vimesajiliwa wawe mabalozi kwa mtu ambaye ameanzisha vituo bila utaratibu kwani  vituo vingi vilivyofungiwa mazingira yake siyo rafiki kwa watoto tundu moja la choo ambalo wanachangia na watu wakubwa na wanao walea ni wale waliomaliza darasa la saba,kidato cha nne na kukosa ajira hawana sifa"alisema  Kibagaya.

Martha  Masota mmiliki wa kituo cha kulelea watoto mchana  kilichopo kata ya Mhongolo  ambacho kimepewa mwezi mmoja kuwa na usajili alisema kuwa amesomea suala la malezi na makuzi (ECD) na muongozo uliopo haitakiwi watoto  hawa kufundishwa kwa kuandika bali zitumike zana ,kuimba na michezo na  kuwepo watoto 25 tu na matundu ya vyoo  na mazingira yawe rafiki.

Mratibu wa kitaifa wa  mtandao wa  malezi ,makuzi  na maendeleo ya awali ya mtoto (TECDEN )Bruno Ghumpi alisema  kweli imebainika watoto  hawa wanapojiunga na vituo vya kulelea watoto  wadogo mchana  huishia katika mfumo  wa kufundishwa  badala ya kujifunza kupitia michezo na kutumia zana kulingana na mazingira yao.

Baadhi ya wazazi  manispaa ya Kahama Jeremiah Ndaki na Mariamu Fadhili walisema kuwa wamekuwa wakiwapeleka watoto wao kwenye vituo hivyo lakini watoto wanakwenda na daftari na kalamu na wamekuwa wakiandika kumbe ni kosa mpaka wafikie umri unaotakiwa.

 

 


J

Post a Comment

0 Comments