Header Ads Widget

RC MJEMA ASHEREHEKEA SIKU YA KUZALIWA RAIS SAMIA NA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI UHURU, AWASISITIZA WASOME KWA BIDII KUTIMIZA NDOTO ZAO


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiimba wimbo wa Happybirthday na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Uhuru Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassani kusherehekea siku yake leo ya kuzaliwa na kutimiza miaka 62 na kumtakia Afya njema.


Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amesherehekea siku ya kuzaliwa Rais Samia Suluhu Hassani kwa kutimiza miaka 62, pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Uhuru Manispaa ya Shinyanga, huku akiwasihi wanafunzi hao wasome kwa bidii ili kutimiza ndoto zao.

Mjema amesherehekea siku hiyo leo Januari 27,2022, ambayo ndiyo Rais Samia Suluhu Hassani ametimiza miaka 62 ya kuzaliwa kwake, kwa kuimba nyimbo ya Happy birthday ya kumpongeza Rais, pamoja na kumtakia Afya njema ili aendelee kuwaongoza Watanzania na kuwaletea maendeleo.

Amesema leo ni siku ya kuzaliwa Rais Samia Suluhu Hassani, hivyo Watanzani hawana budi kusherehekea naye na kufurahi pamoja, kutokana na jinsi anavyo liongoza Taifa vizuri kwa kuwatumikia wananchi, na kuwatekelezea miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Nimekuja hapa shuleni leo, ili tufurahi na wanafunzi kusherehekea siku ya kuzaliwa Rais wetu Samia Suluhu Hassani, kwa kutimiza miaka 62 ya kuzaliwa kwake, pamoja na kumuombea Afya njema kwa mwenyezi Mungu, ili aendelee kuliongoza Taifa,”alisema Mjema.

Pia, amewataka wanafunzi wote mkoani Shinyanga, wasome kwa bidii ili kutimiza ndoto zao, pamoja na kuitunza miundombinu ya ujenzi wa nyumba vya Madarasa, ili waendelee kusoma katika mazingira Rafiki kwa kupata ufaulu mzuri, na kuja hapo baadae kuwa viongozi na watalaam wa Taifa hili.

Aidha amewaagiza Wakuu wa wilaya na Maofisa elimu, kuwachukulia hatua kali wazazi ambao bado wanaendekeza tabia ya kuozesha wanafunzi ndoa za utotoni na kuzima ndoto zao.

Katika hatua nyingine, alisema kwa sasa baada ya kumaliza ujenzi wa vyumba vya madarasa, wameelekeza nguvu kwenye ujenzi wa vituo vya Afya, Miradi ya maji, pamoja na miundombinu ya ujenzi wa barabara.

Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo ya Sekondari Uhuru, akiwamo Paul Kazinga na Flaviana Malya, kwa nyakati tofauti walimpongeza Rais Samia kwa kutimiza miaka 62, pamoja na kuwajengea vyumba vya madarasa, ambapo wanasoma kwa nafasi bila ya kubanana darasani.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiimba wimbo wa Happybirthday na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Uhuru Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassani kusheherekea siku yake  ya kuzaliwa leo na kutimiza miaka 62 na kumtakia Afya njema.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiendelea kuimba wimbo wa Happybirthday na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Uhuru Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassani kusheherekea siku yake ya kuzaliwa leo na kutimiza miaka 62 na kumtakia Afya njema.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Uhuru Manispaa ya Shinyanga wakiimba wimbo wa Happybirthday na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassani kusheherekea siku yake ya kuzaliwa leo na kutimiza miaka 62 na kumtakia Afya njema.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Uhuru Manispaa ya Shinyanga wakiimba wimbo wa Happybirthday na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassani kusheherekea siku yake ya kuzaliwa leo na kutimiza miaka 62 na kumtakia Afya njema.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiswasihi Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Uhuru Manispaa ya Shinyanga wasome kwa bidii ili kutimiza ndoto zao, sababu Rais Samia amewaboreshea mazingira Rafiki ya kusoma, ikiwamo ujenzi wa vyumba vya Madarasa.
Mwanafunzi Paul Kazinga wa Shule hiyo ya Sekondari Uhuru, akimpongeza Rais Samia kutimiza miaka 62 ya kuzaliwa, pamoja na kuwajengea vyumba vya Madarasa ambapo kwa sasa wanasoma kwa kujinafasi bila ya kubanana.

Mwanafunzi Flaviana Malya wa Shule hiyo ya Sekondari Uhuru, akimpongeza Rais Samia kutimiza miaka 62 ya kuzaliwa, pamoja na kuwajengea vyumba vya Madarasa ambapo kwa sasa wanasoma kwa kujinafasi bila ya kubanana.

Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Uhuru Mussa Walelo, akimpongeza Rais Samia kutimiza miaka 62 ya kuzaliwa, na kumtakia Afya njema huku akishukuru kuendelea kuboresha mazingira rafiki ya wanafunzi shuleni, pamoja na utoaji wa Rukuzu elimu bila malipo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments