Header Ads Widget

WAZIRI BASHUNGWA AWATAKA WASANII KUTENGEZA KAZI ZENYE UBORA.

 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Mhe. Innocent akizungumza na wasanii katika hafla fupi iliyoandaliwa na kampuni ya MultChoice Tanzania

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Mhe. Innocent Bashungwa amewataka wasanii wa Tanzania kutumia muda wao vizuri na kuachana na malumbano,  ili kupata muda wa kutengeneza kazi zenye ubora na mvuto kwa watazamaji na wasikilizaji ambazo zitawanufaisha.

Mhe. Bashungwa ametoa kauli hiyo leo Disemba 2, 2021  jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza katika hafla fupi iliyoandaliwa na kampuni ya MultChoice Tanzania kuonesha mafanikio na mipango yake katika Sekta ya Sanaa.

 Aidha, amefafanua kuwa Serikali itaendelea kuwawekea mazingira wezeshi katika kutimiza ndoto zao kupitia tasinia ya sanaa.

 " Watanzania wanahitaji burudani zenye mafundisho na zilizo andaliwa kwa kiwango kinacho ridhisha nashauri wasanii kutumia muda wenu vizuri kuzalisha filamu au kutengeneza muziki unaokidhi vigezo kwa ajili yenu na kwa ajili ya taifa". Amesema Mhe. Bashungwa


  
Baadhi ya wasanii wa filamu walioshiriki hafla iliyoandaliwana  Kampuni ya Multchoice.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Multchoice Tanzania Bi. Jacquiline Woisso ameishukuru Serikali kwa ushirikiano mkubwa inaowapatia katika utendaji wa kazi zao za kila siku.

Aidha, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt. Kiagho  Kilonzo ameiomba Kampuni ya Multchoice Tanzania kupandisha bei ya ununuzi wa filamu akisema baadhi ya wasanii hawako tayari kupeleka filamu zao katika kampuni hiyo kwa madai kuwa gharama ya ununuzi wa filamu zao bado ni ndogo ikilinganishwa na ubora na gharama kubwa zinazotumika kuandaa filamu hizo.

Hafla hiyo fupi imeenda sambamba na uzinduzi wa filamu mbili ambazo ni  tamthilia ya Danga na  la Familia.


Mwisho.

 

 

Post a Comment

0 Comments