Header Ads Widget

JENGO JIPYA KANISA LA EAGT LAWEKWA WAKFU,, VIONGOZI WA DINI WASISITIZWA KUHUBIRI AMANI


Muonekano wa Jingo jipya Kanisa la EAGT Ushirika Manispaa ya Shinyanga ambalo limewekwa Wakfu.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

VIONGOZI wa Dini kutoka Madhehebu mbalimbali hapa nchini, wamesisitizwa kuendelea kuhubiri udumishaji wa amani ya nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, amebainisha hayo leo kwa niaba ya Makamu wa Rais Dk. Philipo Mpango, wakati wa Ibada Maalum ya kuweka wakfu jengo jipya la Kanisa la EAGT, lililopo Ushirika Manispaa ya Shinyanga

Alisema Serikali inatambua kazi kubwa ambayo inafanywa na Madhehebu ya Kidini hapa nchini, kwa kuhakikisha amani na utulivu unatawala ,Tunu ambayo iliasisiwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

"Nipo Kanisani hapa kumwakilisha Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, ambaye yupo kwenye majukumu mengine ya kitaifa, anaomba viongozi wa Madhehebu ya kidini muendele kuhubiri amani ya nchi," alisema Dk. Sengati

"Serikali tunatambua kazi ya viongozi wa dini, ambapo mnaimarisha misingi ya upendo, utu, uzalendo, na mshikamano kwa wananchi, na kuifanya Tanzania kuendelea kuwa na amani na utulivu," aliongeza.

Aidha, alisema Serikali pia inatambua mchango wa madhehebu ya kidini, katika mchango wa kuboresha huduma za Afya, Elimu, na kuahidi kuendelea kuwa unga mkono, huku akilikaribisha kanisa hilo kufanya uwekezaji wa viwanda ambapo watapewa eneo bure.

Katika hatua nyingine Dk. Sengati, aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kupata Chanjo ya UVIKO-19, na kupuuza maneno ya upotoshaji juu Chanjo hiyo, ili siku wakipata maambukizi ya virusi vya Corona wasipate madhara makubwa.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT Dk. Brown Mwakipesile, aliishukuru Serikali kuendelea kutoa uhuru wa kuabudu bila ya kuwapo buguza yoyote ile, na kuahidi kuendelea kuhubiri amani ya nchi.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa Kanisa hilo jipya John Ntalimbo, akisoma taarifa ya ujenzi, alisema ulianza mwaka 2003 na kuisha mwaka huu, kwa gharama ya Sh. Milioni 825.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, akizungumza kwenye Ibada Maalum ya uwekaji Wakfu Jengo Jipya la Kanisa la EAGT.

Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT Dk. Brown Mwakipesile, akiendesha Ibada Maalum ya kuweka wakfu jengo jipya ya EAGT Ushirika Manispaa ya Shinyanga.

Askofu wa Kanisa la EAGT Ushirika Manispaa ya Shinyanga Rafael Machimu, akielezea namna walivyoanza kujenga Jengo hilo jipya la Kanisa.

Mwenyekiti wa Kamati wa Ujenzi wa Jengo hilo Jipya Kanisa la EAGT John Ntalimbo, akisoma taarifa ya ujenzi wa Jengo hilo.

Jiwe la Msingi.

Muonekano wa Jengo jipya Kanisa la EAGT.

Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Ibada Maalum ya kuwekwa Wakfu Jengo Jipya la Kanisa la EAGT.

Waumini wa Kanisa la EAGT Ushirika Shinyanga wakiwa kwenye Ibada Maalum ya uwekaji Wakfu Jengo jipya la Kanisa hilo.

Waumini wa Kanisa la EAGT Ushirika Shinyanga wakiwa kwenye Ibada Maalum ya uwekaji Wakfu Jengo Jipya la Kanisa hilo.

Waumini wa Kanisa la EAGT Ushirika Shinyanga wakiwa kwenye Ibada Maalum ya uwekaji Wakfu Jengo  Jipya la Kanisa hilo.

Waumini wa Kanisa la EAGT Ushirika Shinyanga wakiwa kwenye Ibada Maalum ya uwekaji Wakfu Jengo Jipya la Kanisa hilo.

Waumini wa Kanisa la EAGT Ushirika Shinyanga wakiwa kwenye Ibada Maalum ya uwekaji Wakfu Jengo Jipya la Kanisa hilo.

Wanakwaya wa Kanisa la EAGT Ushirika Shinyanga wakiwa kwenye Ibada Maalum ya uwekaji Wakfu Jengo Jipya la kanisa hilo.

Viongozi wa Serikali na Kanisa la EAGT wakipiga picha ya Pamoja.

Na Marco Maduhu- SHINYANGA

































































Post a Comment

0 Comments