Header Ads Widget

DC MBONEKO KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO STENDI ZA MABASI SHINYANGA


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na viongozi na wafanyabiashara katika Stendi ya Mabasi ya Ibinzamata.


Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

MKUU wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, ameahidi kuendelea kutatua changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwakabili wafanyabiashara pamoja na abiria, katika Stendi za Mabasi Mjini Shinyanga.

Mboneko amebainisha hayo leo, alipofanya ziara ya kutembelea Stendi za Mabasi za Mjini Shinyanga ikiwamo Standi ya Wilaya na Standi ya Mkoa, kwa ajili ya kuona maendeleo ya ukarabati wa vyoo, pamoja na majengo ya kupumzikia abiria.

Alisema Serikali itaendelea kuboresha mazingira mazuri kwenye stendi hizo za Mabasi, ili wafanyabiashara wafanye biashara zao katika mazingira mazuri, pamoja na abiria kupumzika sehemu zenye kivuli wakati wakisubiri mabasi.

“Nimefanya ziara katika Stendi za Mabasi kuona ukarabati ambao umefanyika wa ujenzi wa vyoo, pamoja majengo ya kupumzika abiria, na pale penye changamoto tutaendelea kuzitatua,”alisema Mboneko.

“Katika Stendi hii kuu ya Mabasi ya Ibinzamata, mbali na kukarabati choo hiki, pia tutajenga choo kingine kikubwa cha kisasa, kulikarabati jengo la kupumzikia abiria, pamoja na kufunga Taa zitakazotumia umeme wa jua (Solar), ili usiku pawe na Mwanga,”aliongeza.

Pia, amewataka wafanyabiashara wa Stendi hizo mbili pamoja na abiria, kutunza usafi wa mazingira na kuacha kujisaidia haja ndogo kwenye makopo, bali wavitumie vyoo ambavyo vimejengwa na kuimarisha usafi.

Naye Mwenyekiti wa Stendi ya Mabasi Ibinzamata Khobe Marwa, amempongeza mkuu huyo wa wilaya kwa kukarabati choo cha Standi hiyo, ambapo awali kilikuwa katika hali mbaya, lakini kwa sasa kipo katika mazingira mazuri na kulinda usalama wa afya zao.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na viongozi na wafanyabiashara katika Stendi ya Mabasi ya Ibinzamata.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikagua jengo la kupumzikia abiria katika Stendi ya Mabasi wilaya, ambalo linaendelea kupakwa rangi.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikagua ukarabati wa ujenzi wa Choo cha Mabasi ya wilayani.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikagua ukarabati wa Karo katika Stendi ya Mabasi ya wilaya.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikagua ukarabati ujenzi wa Choo cha Stendi ya Ibinzamata.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikagua ukarabati ujenzi wa Choo cha Stendi ya Ibinzamata.

Na Marco Maduhu-SHINYANGA.















































Post a Comment

0 Comments