Header Ads Widget

ASKARI WALIOMUUA HAMZA WAPEWA ZAWADI YA PESA


JESHI la Polisi nchini limewapa zawadi askari Polisi walipambana na kumuua mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Hamza Mohammed mkazi wa Upanga, Dar es Salaam aliyejihami kwa silaha na kuua askari polisi watatu na mlinzi mmoja wa Kampuni ya SGA.


Hayo yamesemwa leo Jumatatu, Septemba 20, 2021 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam akizungumzia tukio hilo lililotokea Agosti 25, 2021 katika jirani na ulipo Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam.


“Askari hawa (Waliopambana na Hamza) miongoni mwao walikuwa ni Askari 11, ambao kwa mamlaka za kisheria za uendeshaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP amewapa zawadi ya vyeti vya ujasiri na zawadi ya pesa kwa kadri alivyoona inafaa.


“Askari Polisi walipambana kuhakikisha kwamba madhara makubwa zaidi ya yale yaliyotokea hayatokei, nani ambaye hafahamu kama yule mhalifu angeondoka na zile silaha zilizokuwa na magazine 2 na risasi 60 na zingine alizokuwa nazo nini kingefanyika.

SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MALUNDE I BLOG

Post a Comment

0 Comments