Header Ads Widget

WAANDISHI WA HABARI WAPEWA MAFUNZO KUANDIKA HABARI ZA CORONA

Mwenyekiti wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika,Tawi la Tanzania (MISA-TAN) Salome Kitomari akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari.

Na Marco Maduhu, Morogoro

WAANDISHI wa habari kutoka vyombo mbalimbali, wamepewa mafunzo namna ya kuandika habari zinazohusu maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19).

Waandishi hao ni kutoka Mkoa wa Morogoro, Dar es salaam, Njombe, Mtwala, Pwani, Manyara, Arusha, Mbeya Shinyanga,Mara, na Njombe, ambayo yata dumu siku Tano mkoani Morogoro, yaliyoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika,Tawi la Tanzania (MISA-TAN), kwa kushirikiana na Shirika la Ujerumani la IDEM kwa ufadhili wa Shirika la misaada la kijerumani (GIZ).

Akizungumza leo wakati wa kutoa mada ya mambo ya kuzingatia taaluma ya habari, Mwenyekiti wa MISA-TAN, Salome Kitomari aliwataka wanahabari kuzingatia weledi wa taaluma yao wakati wa kuandika habari zinazohusu Corona.

Alisema waandishi wa habari wanapaswa kuwa makini katika uandishi wao, ili kuepuka kuleta taharuki, bali waandike habari ambazo ni za kweli, zilizozingatia maadili ya taaluma yao.

"Nawaomba waandishi wa habari tunapoandika habari hizi za Corona, tuzingatie maadili ya taaluma, tutafute vyanzo sahihi vya habari, tuzingatie utu, na tuepuka hotuba za uchochezi," alisema Kitomari.

Naye, Mwandishi wa habari Mwandamizi Sammy Awami, akitoa soma la haki za binadamu, amewataka waandishi habari kuzingatia pia makundi maalumu wakati wa kuandika habari za Corona.

Awali, Daktari wa Magonjwa ya ndani kutoka Hospital ya Rufani mkoani Morogoro Abilay Issa, amewataka waandishi wa habari, wanapokuwa katika majukumu yao kuwa makini na kujikinga na virusi hivyo kwa kuvaa vifaa kinga ili kuepuka kuambukizwa au kusambaza.

Pia, amewataka wananchi pale wanapokuwa wakiona dalili za kupata maambukizi ya virusi vya Corona, wawahi kwenye huduma za kiafya, ili kupata matibabu mapema, na siyo kusubili kuwa katika hali mbaya au kutumia dawa wanazosikia mtandaoni au kupewa na marafiki.

Aidha,amezitaja dalili za maambukizi ya virusi vya Corona awamu ya tatu, kuwa ni kupata homa kali, mwili kuchoka, kushindwa kupumua, kichwa kuuma, kuhara, pamoja na kutapika.


Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika,Tawi la Tanzania (MISA-TAN) Salome Kitomari akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari.


Mwandishi wa habari Mwandamizi Sammy Awami, akitoa soma la haki za binadamu, na Corona kwenye mafunzo hayo ya waandishi wa habari.


Daktari wa Magonjwa ya ndani kutoka Hospital ya Rufani mkoani Morogoro Abilay Issa, akitoa mafunzo wa waandishi wa habari.
 Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo juu ya kuandika habari za Corona.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo juu ya kuandika habari za Corona.
 
Na Marco Maduhu- Morogoro.








Post a Comment

0 Comments