Header Ads Widget

RAIS SAMIA ACHANJWA CHANJO YA CORONA, ATOA UJUMBE MZITO KWA WATANZANIA


Rais Samia Suluhu Hassan amesema asingekuwa tayari kuhatarisha maisha yake kwa kuchanjwa chanjo ya covid kama ingekuwa si salama.


Rais Samia ameyasema hayo leo Jumatano Julai 28, 2021 katika uzinduzi wa uchanjaji wa chanjo hiyo, hafla iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam.

Hatua hiyo inakuja baada ya wiki iliyopita Tanzania kupokea zaidi ya dozi milioni 1.05 za chanjo aina ya Johnson & Johnson zilizotolewa na Marekani kupitia mpango wa upatikanaji wa chanjo Covax.

Katika mpango huo, wapo baadhi ya watu wanaopingana na harakati hizo wakieleza chanjo hizo sio salama na wapo wanaounga mkono, lakini kiongozi huyo mkuu wa nchi amewaondoa hofu wananchi kuhusiana na hilo.

Rais Samia alisema yeye ni mama wa watoto wanne, ni bibi wa wajukuu kadhaa wanaompenda sana na yeye kuwapenda, ni mke pia lakini mbali ya yote ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi wa nchi hii.

“Nategemewa kama mama, kama bibi, kama Rais, kama Amiri Jeshi Mkuu, nisingejitoa mwenyewe nikajipeleka kwenye kifo, nikajipeleka kwenye hatari nikijua kwamba nina majukumu yote haya yananitegemea .

 SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANANCHI

 

Post a Comment

0 Comments