Header Ads Widget

KATAMBI AZINDUA MRADI WA MAJI SHULE YA SEKONDARI KOLANDOTO


Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira, mwenye kofia, akikata utepe kuzindua mradi wa maji wa kisima kirefu katika shule ya Sekondari Kolandoto.Na Marco Maduhu, Shinyanga.


Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, amezindua mradi wa maji wa kisima kirefu, katika shule ya Sekondari Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
 
Zoezi la uzinduzi wa mradi huo limefanyika leo katika shule hiyo, na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, na chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, wakiwamo wanafunzi na wananchi.

Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira, amesema mradi huo utasaidia wanafunzi kutunza mazingira ya shule kwa kupanda miti, pamoja na usafi.

"Mpaka sasa nimesha chimba visima viwili vya maji katika shule za Sekondari, ya Mwawaza na hapa Kolandoto, ili kumaliza tatizo la wanafunzi kukosa maji shuleni, na hili nitalifanya kwenye shule zote ambazo zina changamoto ya ukosefu wa maji," amesema Katambi.

Aidha amewataka wanafunzi kuendelea kusoma kwa bidii, ili watimize ndoto zao, huku akiahidi kuzifanyia kazi changamoto zote katika shule hiyo, ikiwamo ya upungufu wa mtundu ya choo, Walimu, Viti, Meza, na Nishati ya umeme.

Nao baadhi ya wanafunzi wa Shule hiyo akiwamo Magesa Rubinza na Salma Abdul, kwa nyakati tofauti wamesema mradi huo wa maji utakuwa mkombozi kwao, hasa katika utunzaji wa mazingira na usafi, na kuepukana na magonjwa ya mlipuko.

Pia wamesema mradi huo wa maji umewapusha kupoteza muda wa masomo kwa kufuata maji umbari mrefu, pamoja na kubeba maji kutoka nyumbani na kufika shuleni wakiwa wameshachoka, na kutokuwa makini na masomo.

Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu, amempongeza Mbunge Katambi kwa kazi nzuri ambayo anaifanya, ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho kwa vitendo.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kolandoto Deus Maganga, amesema mradi huo wa maji ni mkombozi katika shule hiyo, kwa utunzaji wa mazingira na usafi, na hata kuondoa adha ya wananchi ya ukosefu wa maji, ambao anaishi jirani na shule hiyo, ambapo wamekuwa wakiyatumia.

Amesema mradi huo ulianza kutekelezwa June 8 mwaka huu, na kukamilika June 12, kwa gharama ya Sh.milioni 20, kwa msaada wa Ofisi ya Mbunge Katambi, chini ya mfadhili Serving Friends International kutoka Arusha.

TAZAMA PICHA HAPA CHINIMbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira, akizungumza na wanafunzi katika Shule ya Sekondari Kolandoto.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira, akizungumza na wanafunzi katika Shule ya Sekondari Kolandoto.

Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu, akizungumza katika shule hiyo ya Kolandoto.
Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew akizungumza kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa mradi wa maji.

Mtendaji wa Kata ya Kolandoto Wilison Mwakaluba,akizungumza kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa mradi wa maji.

Katibu wa umoja wa vijana wa CCM, UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Raphael Nyandi, akizungumza kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa mradi wa maji katika shule ya Sekondari Kolandoto.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kolandoto, Deus Maganga, akisoma taarifa ya mradi huo wa maji shuleni hapo.

Mwanafunzi Salma Abduli akielezea umuhimu wa mradi huo wa maji shuleni hapo.

Mwanafunzi Magesa Lubinza akielezea umuhimu wa mradi huo wa maji shuleni hapo.

Wanafunzi shule ya Sekondari Kolandoto wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa kisima kirefu cha maji shuleni hapo.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira, mwenye kofia, akikata utepe kuzinduz mradi wa maji wa kisima kirefu katika shule ya Sekondari Kolandoto.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira, akipampu maji kwenye kisima hicho cha maji katika shule ya Sekondari Kolandoto.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kolandoto wakiwa kwenye kisima cha maji shuleni hapo.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, na Ajira, awali akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili kuzindua kisima cha maji katika shule ya Sekondari Kolandoto.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.Post a Comment

0 Comments