Header Ads Widget

KANISA LA KKKT DAYOSISI KUSINI MASHARIKI YA ZIWA VICTORIA LASIMIKA VIONGOZI WAPYAAskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akimungiza kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu (katikati)

Na Kadama Malunde- Malunde 1 blog

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala ameongoza Ibada ya Kuingizwa Kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu na kusimika Wakuu wa Majimbo 9 ya Dayosisi hiyo.

Askofu Makala pia ameongoza ibada ya kuingizwa kazini wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Dayosisi, kubariki wachungaji wawili ambao ni Joseph Nkangala na Hubert Teghama na kuaga wajumbe wa halmashauri kuu waliomaliza muda wao wa miaka nane kazini.

Ibada hiyo imefanyika leo Jumapili Februari 14,2021 katika kanisa Kuu la KKKT Ebenezer Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Daudi Talaba kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack.

Akizungumza katika ibada hiyo, Askofu Makala  aliwataka viongozi waliosimikwa na kuingizwa kazini kuzingatia  taratibu za kanisa katika uongozi wao.

Askofu Makala pia ametumia fursa kuwakumbusha wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona na magonjwa mengine yanayoambukizwa kwa njia ya uchafu huku akiwataka wananchi wa mkoa wa Shinyanga kutumia mvua zinazonyesha kulima mazao mbalimbali na kupanda miti.

Aidha ameipongeza serikali kwa kuheshimu na kutoa ushirikiano kwa viongozi wa dini huku akiiomba serikali kufanyia kazi  ombi la kujenga Uwanja wa ndege, soko la kisasa na stendi ya kisasa mkoani Shinyanga ili kupiga hatua zaidi kimaendeleo.

Naye Msaidizi wa Askofu, Mchungaji Yohana Ernest Nzelu aliwashukuru wajumbe wa halmashauri kuu kumteua kuwa Msaidizi wa Askofu akichukua nafasi ya Mchungaji Trafaina Nkya ambaye amestaafu huku akiahidi  kulitumikia kanisa kwa kufanya kazi kwa unyenyekevu, utii na ujasiri.

Pai aliiomba serikali kulitafutia ufumbuzi suala la ukosefu wa ajira kwa vijana wanaotoka vyuoni.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Talaba akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack aliwapongeza viongozi wa wapya wa kanisa na kueleza kuwa serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na viongozi wa dini ikiwemo kulinda amani ya nchi,kujenga miundombinu ya afya,elimu na kutekeleza miradi mbalimbali.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akizungumza wakati wa Ibada ya Kuingizwa Kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu na kusimika Wakuu wa Majimbo 9 ya Dayosisi hiyo na wajumbe wa halmashauri kuu leo Jumapili Februari 14,2021 katika kanisa Kuu la KKKT Ebenezer Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Daudi Talaba akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack wakati wa Ibada ya Kuingizwa Kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu na kusimika Wakuu wa Majimbo 9 ya Dayosisi hiyo na wajumbe wa halmashauri kuu leo Jumapili Februari 14,2021 katika kanisa Kuu la KKKT Ebenezer Mjini Shinyanga.

Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Happiness Gefi akitoa maelekezo wakati wa Ibada ya Kuingizwa Kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu na kusimika Wakuu wa Majimbo 9 ya Dayosisi hiyo na wajumbe wa halmashauri kuu leo Jumapili Februari 14,2021 katika kanisa Kuu la KKKT Ebenezer Mjini Shinyanga.

Ibada ikiendelea

Ibada ikiendelea

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akimungiza kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu (kulia)

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akimungiza kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu (katikati)

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akimungiza kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akimkabidhi Biblia Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu (kulia)

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akimkabidhi Mwongozo wa Kanisa Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu (kulia)

Ibada ya kumuingiza Kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu (kulia) ikiendelea

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akimpongeza Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu (kulia) baada ya kumuingiza kazini

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala na Wachungaji wakimuombea Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akimpongeza Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu (kushoto)

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akimtambulisha kwa washarika Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu (kushoto)

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akimuombea Mke wa Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu, Bi. Lilian

Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu akipongezana na mke wake

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akimtambulisha Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Yohana Ernest Nzelu (wa pili kushoto) kwa Uongozi wa Mkoa wa Shinyanga (Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Talaba (kulia) aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akizungumza kanisani. Kulia ni Mchungaji Trafaina Nkya ambaye amestaafu nafasi ya Msaidizi wa Askofu kanisa hilo.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Talaba (kushoto) aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack akiwa kanisani.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akiwaingiza kazini Wachungaji 9 wapya wa Majimbo katika Dayosisi hiyo.

Kwaya ya Kanisa la KKT Shinyanga ikiimba

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akiwaingiza kazini Wajumbe wa Halmashauri Kuu

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akiwaingiza kazini Wajumbe wa Halmashauri Kuu

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akiwabariki Wajumbe wa Halmashauri Kuu

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akiwaingiza kazini Wajumbe wa Halmashauri Kuu

Wajumbe wa Halmashauri Kuu wakiwa kanisani

Wajumbe wa Halmashauri Kuu wakigeukia washarika

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akiwaaga Wajumbe wa Halmashauri Kuu ambao muda wao umemalizika
Wachungaji wa Kanisa la KKKT wakiwa kanisani

Wachungaji wakiwa kanisani

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dk. Emmanuel Joseph Makala akiwaingiza kazini Mashemasi wawili ambao ni Joseph Nkangala na Hubert Teghama (kuli) kuwa Wachungaji

Kushoto ni Mchungaji Trafaina Nkya (aliyestaafu nafasi ya Msaidizi wa Askofu) akiteta jambo na Mchungaji Yohana Ernest Nzelu ambaye Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria

TAZAMA PICHA ZAIDI <<HAPA>>

Picha : KANISA LA KKT DAYOSISI KUSINI MASHARIKI YA ZIWA VICTORIA LAPATA MSAIDIZI WA ASKOFU MPYA, WACHUNGAJI WA MAJIMBO NA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU

TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807