Header Ads Widget

JPM AMSAMEHE MKURUGENZI KAHAMA NA KUMRUDISHIA GARI, SASA YAPANDISHWA HADHI KUWA MANISPAARais Dk. John Pombe Magufuli

Na Damian Masyenene
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli ameamua kumsamehe na kumrudishia gari, Mkurugenzi wa Mji wa Kahama, Anderson Msumba, huku akiupandisha hadhi mji huo kuwa manispaa.

Mkurugenzi huyo ni miongoni mwa wakurugenzi wanne waliokuwa hatiani kwa kununua magari ya kifahari, ambapo Rais Magufuli ameeleza kuwa kutokana na kazi kubwa aliyoifanya mkurugenzi huyo katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa hospitali ya mji huo, ameamua kumsamehe na sasa yuko huru kuendelea kulitumia gari hilo.

JPM ametoa msamaha huo leo Januari 28, 2021 katika mkutano wake kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama, ambapo mbali na msamaha huo, ameupandisha hadhi mji wa kahama kuwa manispaa.

Vile vile amemuagiza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Doroth Gwajima kuipandisha hadhi hospitali ya Mji  Kahama iendane na hadhi ya Manispaa.

"Nimemsamehe Mkurugenzi huyu, amefanya makubwa! Mkurugenzi hongera Sana. Na hilo gari nitamrudishia aendelee kuliendesha lakini asirudie kununua gari nje ya utaratibu.

"Kwa sababu mimi ndiye Rais na mmenichagua, basi ninaipandisha iwe Manispaa, najua Shinyanga hawana raha lakini Mimi nataka maendeleo, hii miradi imenigusa sana

"Nawaongezea Sh Milioni 500 kuchangia jengo la hospitali ya mji Kahama. Na kwa vile waziri wa afya yuko hapa aipandishe hadhi hiyo hospitali ili endane na hatua ya Manispaa," amesema JPM.

Post a Comment

0 Comments