Header Ads Widget

ALIKIBA: NILISHAVUKA UMRI WA KUVAA HERENI MASKIONI

Msanii Alikiba

Nyota wa muziki wa Bongofleva Alikiba ambaye jana Jumatatu Januari 18, 2021, aliachia ngoma yake mpya inayoitwa Infidele, amesema suala la uvaaji kwenye video zake halimsumbui tena maana mambo mengi ameshayapitia.

Amefunguka hayo leo Januari 19, 2021 kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, ambayo huruka Jumatatu mpaka Ijumaa saa 7:00 mchana hadi saa 10:00 jioni.

''Mambo ya kuvaa sijui hereni masikioni na vitu vingine vya aina hiyo, nadhani kwangu muda wake ulishapita.Hata mitindo yangu ya sasa kuanzia uvaaji wangu kwenye video nadhani unafaa kwasababu watu wanaohusika na ubunifu wanafanya kazi yao'' - Alikiba

Aidha mkali huyo ameongeza kuwa, ''Mimi nilishafanya kila kitu ikiwemo kuvaa sana kuendana na trend lakini hivi sasa nimeacha hayo mambo kwasababu muda ukishapita umepita inabidi uwe na vitu vipya pia''.
TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807