Header Ads Widget

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA WAZIRI MKUU, WAZIRI MAMBO YA NJE NA WAZIRI WA FEDHA



Rais John Magufuli amemuapisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na mawaziri wengine wawili ambao ni Waziri wa Fedha Dk. Philip Mpango na Waziri wa Mambo ya Nje, Profesa Palamagamba Kabudi.

Akihutubia katika hafla fupi iliyofanyika leo asubuhi jijini Dodoma, Rais Magufuli amesisitiza kwamba kuteuliwa kwa Majaliwa kuwa Waziri Mkuu kwa awamu ya pili haina maana ni nafasi ya uhakika moja kwa moja bali, 'itategemea utendaji wake' rais alisema.

Akihutubia katika hafla fupi iliyofanyika leo asubuhi jijini Dodoma, Rais Magufuli amesisitiza kwamba kuteuliwa kwa Majaliwa kuwa Waziri Mkuu kwa awamu ya pili haina maana ni nafasi ya uhakika moja kwa moja bali, 'itategemea utendaji wake' rais alisema.

Uteuzi huu wa mapema unachukuliwa kama ishara kwamba Rais Magufuli yuko mbioni kutekeleza ahadi zake za kampeni pamoja na vipaumbele vyake vya maendeleo kama alivyo orodhesha kwenye hafla ya uapishwaji wake.

Kwenye hutuba yake siku akiapishwa kuingia ikulu kwa mara ya pili kama rais wa Tanzania, Rais Magufuli alisema kwamba, mara tu baada ya usalama wa taifa, kipaumbele chake kikubwa ni maendeleo ya uchumi. Kipaumbele hicho kikosambamba na uteuzi wake wa Waziri wa Fedha.

Pia rais alikaribisha uwekezaji wa kigeni katika sekta tofauti na kusisitiza pia ujenzi wa mahusiano wa kimataifa, kipaumbele hichi pia kimeenda sambamba na uteuzi wake wa pili wa waziri, Waziri wa Mambo ya nje.

Rais pia alitumia hutuba hiyo kuwaonya wabunge ambao wanataka uteuzi wa uwaziri. Alionya kuwa hakuna kiti cha uwaziri kitakachokuwa rahisi lakini badala yake, wote watahitajika kufanya kazi kwa bidii na kutekeleza majukumu yao.

Post a Comment

0 Comments