Header Ads Widget

WALIOHARIBU MALI ZA WAGOMBEA WA CHADEMA CHATO KUKIONAKamanda wa polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe

Polisi mkoa wa Geita, linawasaka watu zaidi ya 10 waliofanya uharibifu wa mali kwenye nyumba 3 tofauti za wagombea Udiwani na Ubunge jimbo la Chato kupitia CHADEMA, waliovamiwa usiku wa kuamkia Oktoba 13, 2020, ambapo walikuwa wanatarajia kumpokea mgombea Urais wa chama hicho, Tundu Lissu.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe, na kutaja mali zilizoharibiwa kuwa ni pamoja na bajaji mbili kuchomwa moto, kuvunjwa kwa vioo vya madirisha baada ya kupondwa mawe, pamoja na kubomoa madirisha mawili ya nyumba.

Kwa upande mwingine Kamanda huyo amewasisitiza wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi, kuzingatia muda wa kufanya kampeni ili kuepusha vurugu zinazotokea baada ya muda uliowekwa na Tume kuisha. 

CHANZO: EATV 


Post a Comment

0 Comments