Header Ads Widget

DK. MWINYI KUKIPANDISHA HADHI KITUO CHA AFYA MICHEWENI KUWA HOSPITALI, KUONGEZA WALIMU WA SAYANSI

LEO Oktoba 15, 2020 Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi amefanya mkutano wake wa kampeni kisiwani Pemba katika uwanja wa Shaame Mata, Micheweni, ambapo pamoja na mambo mbalimbali ameahidi kukipandisha hadhi kituo cha afya Micheweni na kuwa hospitali endapo atachaguliwa kuwa Rais wa awamu ya Nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Pia ameahidi kuongeza walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati katika shule za sekondari ili kupunguza uhaba uliopo.

Tazama hapa chini baadhi ya ahadi zingine alizozitoa leo Dk. Hussein MwinyiUSHINDI WA MAPEMA Zanzibar: Aliyoyazungumza Mgombea Urais kupitia CCM wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi Leo Oktoba 15, 2020 Kwenye Mkutano wa Kampeni Uliofanyika Viwanja Vya Shaame Mata, Micheweni, Pemba.
#YajayoniNeematupu#Mwinyi2020 


Post a Comment

0 Comments