Header Ads Widget

TAKUKURU YATOA TAMKO WANAORUBUNI WANANCHI VITAMBULISHO VYA KUPIGIA KURA


Picha na Mwananchi

Na Shinyanga Press Club Blog

KUTOKANA na kuripotiwa kuwepo kwa vitendo vya baadhi ya watu kuwarubuni wananchi kupitia vitambulisho vya kupigia kura kwa kupewa fedha na kuuza kadi hizo, hatimaye taarifa hizo zimeifikia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambayo imeingilia kati na kutoa onyo kwa watu wenye nia ovu kwani wanawaondolea wananchi haki ya msingi ya kikatiba.

Akitolea taarifa juu ya jambo hilo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Afisa Uhusiano wa TAKUKURU, Doreen Kapwani amewataka wanaojihusisha na vitendo hivyo waache mara moja kwani wakikamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Soma zaidi hapa chini taarifa hiyo kutoka Takukuru




Post a Comment

0 Comments