Header Ads Widget

NEEMA LUGANGIRA ATEULIWA KUWA MLEZI WA CCM WILAYA YA BUKOBA



MBUNGE Mteule Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania (CCM) Neema Lugangira akizungumza na wenyeviti wa serikali za mitaa kata ya Kahororo kulia ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Bilele Bushira Jumanne


MBUNGE Mteule Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania (CCM) Neema Lugangira ameteuliwa kuwa mlezi wa Chama cha Mapinduzi kata za Kahororo na Nshambya wilaya ya Bukoba mjini.
 
Uteuzi huo umefanywa na Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Bukoba Mjini na leo Septemba 26 mwaka huu baada ya kupokea barua ya kutaarifiwa juu ya majukumu hayo, tayari mlezi huyo amekwisha kuanza kampeni za kisayansi kata hizo mbili zilizopo kwenye Jimbo la Bukoba mjini.




Akizungumza na waandishi wa habari Lugangira amesema kwamba kwa kutambua ukaribu wao na jamii, aliona ni vyema kabla ya kupanga mikakati ya kisayansi akutane na wenyekiti wa serikali za mitaa yote kwenye kata hizo mbili. 

Alisema lengo la kukutana nao ni kupata tathimini ya hali halisi kwa mtizamo wao na kupata uelewa wa maeneo gani ambayo kwa kushirikiana wanaweza kuweka mikakati ya kisayansi . 

Lakini pia kuwasilisha kwao mawazo yangu ya awali ili niweza kupata maoni yao na sasa baada ya kukutana nao kwa nafasi yao yenye umuhimu mkubwa sana nitakutana na viongozi wenzangu CCM na Jumuiya za UWT, UVCCM na Wazazi ngazi za Wilaya, Kata na Matawi kwa lengo la kuweka mikakati ya Kisayansi ambayo nitairatibu” Alisema.
 
Aidha alisema kwamba jitihada hizo zinaenda sanjari na jitihada zingine ambapo kwa ujumla watahakikisha Chama Cha Mapinduzi kinapata ushindi wa kishindo kwa upande wa Urais, Wabunge na Madiwani kwenye uchaguzi mkuu ujao. 

Kwa upande wa Jimbo la Bukoba Mjini nimepangiwa pia mitaa miwili ya Kata za Kashai huku Kata ya Kahororo ikiwa na mitaa mitano na kata ya Nshambya ikiwa na mitaa mitatu" Alisema 

Hata hivyo alisema kwamba katika kipindi cha kampeni sambamba na kukutana na makundi ya NGOs mbalimbali ataendesha kampeni za kisayansi katika mitaa 10 aliyopangiwa kati ya 66 ndani ya Jimbo la Bukoba Mjini.


MBUNGE Mteule Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania (CCM) Neema Lugangira akizungumza na wenyeviti wa serikali za mitaa

MBUNGE Mteule Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania (CCM) Neema Lugangira akisikiliza mawazo ya wenyeviti wa serikali za mitaa 
MBUNGE Mteule Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania (CCM) Neema Lugangira akisisitiza jambo kwa wenyeviti wa serikali za mitaa
MBUNGE Mteule Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania (CCM) Neema Lugangira akisikiliza maoni ya wenyeviti wa serikali za mitaa
MBUNGE Mteule Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania (CCM) Neema Lugangira   kushoto akichukua mawazo ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa

MBUNGE Mteule Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania (CCM) Neema Lugangira katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa kata ya Nshambya 
MBUNGE Mteule Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania (CCM) Neema Lugangira katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa wa Kata ya Kahororo