Header Ads Widget

TFF YAMFUNGIA MIAKA 2 NA FAINI YA SH. MILIONI 8 ALIYEKUWA KOCHA WA YANGA



Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael

LEO Agosti 3, 2020 Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemfungia miaka miwili na kumtoza faini ya Sh Milioni 8 aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mbelgiji Luc Eymael.

Adhabu hiyo imekuja kutokana na kikao cha Kamati ya Nidhamu ya TFF kilichoketi leo Jijini Dar es Salaam.

"Kamati ya Nidhamu ya TFF imemfungia Kocha Luc Eymael miaka miwili na kumtoza faini ya jumla ya shilingi milioni 8 kwa kosa la uchochezi na ubaguzi," imenukuliwa TFF.