Header Ads Widget

AYOUB LYANGA WA COASTAL UNION NAYE ATUA AZAM FC


Ayoub Lyanga (kulia) akitambulishwa rasmi kuwa mchezaji wa Azam FC

KALBU ya Azam FC 'Wana Lamba Lamba' imeendelea kuboresha kikosi chake na kuifanyia kazi ripoti ya kiufundi ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba kwa kufanya usajili, ambapo leo Agosti 2, 2020 imefanikiwa kuingia mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji wa Coastal Union ya Tanga, Ayoub Lyanga.

Lyanga mabye amehusika katika magoli 16 ya timu yake msimu uliomalizika akipachika magoli 8 na kusaidia mengine 8 (assist) anakuwa mchezaji wa pili kuondoka ndani ya Coastal Union baada ya jana Beki kisiki wa timu hiyo, Bakari Nondo Mwamnyeto kusainiwa na Yanga SC.

Mbali na Lyanga, tayari matajiri hao wa Azam wamekwishakamilisha usajili wa wachezaji wawili ambao ni Ally Niyonzima kutoka Rayon Sports ya Rwanda na Awesu Awesu kutoka Kagera Sugar.