Header Ads Widget

WAZIRI HASUNGA ATOA SIKU 14 KWA MKURUGENZI WA BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO KUKAMILISHA MALIPO YA WAKULIMA WA KOROSHO

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye maonesho ya kilimo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo-TARI SERIAN Jijini Arusha
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akikagua shamba la maharage wakati alipotembelea Jijini Arusha kufungua maonesho ya kilimo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo-TARI SERIAN Jijini Arusha
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akikagua shamba la mahindi yaliyozalishwa kwa kutumia mbolea ya Minjingu wakati alipotembelea Jijini Arusha kufungua maonesho ya kilimo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo-TARI SERIAN Jijini Arusha
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akikagua bidhaa mbalimbali za maharage wakati alipotembelea Jijini Arusha kufungua maonesho ya kilimo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo-TARI SERIAN Jijini Arusha
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akikagua mazao mbalimbali ya mizizi wakati alipotembelea Jijini Arusha kufungua maonesho ya kilimo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo-TARI SERIAN Jijini Arusha

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha

Rais wa awamu ya tatu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Benjamini Mkapa wakati wa utawala wake aliainisha kuwa

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amebainisha hayo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye maonesho ya kilimo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo-TARI SERIAN Jijini Arusha na kuongeza kuwa Mkapa alieleza dhamira ya serikali kuhakikisha kuwa inafikia 

“Hayati Rais Mkapa wakati wa utawala wake alilisisitiza kuwa nchi yoyote ili iwe na Usalama na Amani ni lazima wananchi wawe wamejitosheleza kwa chakula endapo kutakuwa na upungufu wa chakula ni dhahiri kuwa nchi haiwezi kuwa na utulivu wa kisiasa na kimaendeleo’’ Alisema

Pia Hayati Mkapa alipiga vita kwa nguvu kubwa umasikini ambapo alianzisha kauli mbiu ya MTAJI WA MASIKINI NI NGUVU ZAKE MWENYEWE ikilenga kuhamasisha wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kuchagiza shughuli za maendeleo.

Kadhalika Hayati Benjamin Mkapa alisisitiza ulazima wa maafisa Ugani kufanya kazi mashambani kwa wakulima badala ya kuishi mjini pekee kwani kwa kufanya hivyo watawasaidia wananchi kunufaika na kilimo kwa kuwa na tija kubwa katika uzalishaji hivyo kuwa na kilimo cha kibiashara.

Waziri Hasunga amesema kuwa Hayati Rais Mkapa alikuwa muumini wa teknolojia bora za kilimo hivyo aliitaka Wizara ya Kilimo kuhakikisha kuwa inatumia teknolojia na zana bora za kilimo ili kuhakikisha kuwa malighafi zinazotokana na mazao ya kilimo zinaendelea kuzalishwa kwa wingi.

Kadhalika, Hayati Mkapa alisema kuwa kilimo bila utaalamu hakiwezi kumkomboa mkulima hivyo aliagiza Taasisi za utafiti wa Kilimo na vyuo vya mafunzo ya ufundi kuhakikisha kuwa vinaendeleza juhudi za kuimarisha elimu kwa wananchi na wakulima ili kuwa na taifa bora lenye wakulima wazuri.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments