Header Ads Widget

JAQULINE KISANGA ATOA NENO BAADA YA KUCHUKUA FOMU YA UBUNGE NYAMAGANA


Jaquline Kisanga akizungumza baada ya kuchukua fomu
BAADA ya Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza kumuunga mkono kwa kumsindikiza kuchukua fomu ya kuwania ubunge wa jimbo hilo, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama hicho (BAWACHA) mkoa wa Mwanza, Jaquline Kisanga, ametaja vipaumbele vyake, huku akiwahimiza wenzake kuacha uoga kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao.
Mwenyekiti huyo wa Bawacha Mwanza alisindikizwa na wanachama na viongozi wa Bawacha Nyamagana kuchukua fomu Julai 9, 2020 katika ofisi za Chadema Kanda ya Viktoria, ambapo baadhi ya wanawake waliojitokeza kumsindikiza akiwemo Majona Zacharia ambaye ni Katibu wa Baraza la Wanawake Isamilo na Veneranda Dioniz ambaye ni Katibu wa BAWACHA kata ya Nyamagana, wamesema kuwa ifike wakati sasa wanawake waweze kujisimamia na kuthubutu kugombea nafasi za uongozi huku wakiwatoa hofu wanawake wengine.
“Viongozi wote watakaohitaji kuchukua fomu wasisite kutuambia kama wanahitaji msaada wa wanawake, sisi tutaungana nao kwa sababu sisi ni jeshi kubwa, na mimi kama kiongozi wao kwa Nyamagana niko tayari kushirikiana na viongozi wote wanaohitaji msaada wetu,” amesema Veneranda.
Kwa upande wake, Jaquline Kisanga baada ya kuchukua fomu ya kuwania jimbo hilo, amesema chama chake kikimpa ridhaa ataanza na miundombinu ya bararabara na changamoto za wanawake wanazokumbana nazo wakati wa kujifungua.
“Endapo chama change kitanipa ridhaa ya kukiwakilisha kwenye jimbo la Nyamagana, kwanza kabisa kipaumbele change kitakuwa ni miundombinu kwa sababu akina mama ndiyo wanaoteseka zaidi na miundo mbinu mibovu, pia kuhakikisha natatua changamoto zinazowakumba wakati wa kujifungua.
Tutawaondolea usumbufu wanaoupata wakati wa kujifungua ikiwemo kutakiwa kwenda na vifaa vya kujifungulia wakati wengine hawana uwezo wa kununua,pia miundombinu ya barabara nyingi za nyamagana ni mibovu nitaanza kuirekebisha ili iweze kupitika kwa urahisi na isilete usumbufu hasa nyakati za mvua,” amesema.
Jaquline akitoka katika ofisi za chama chake kuchukua fomu
 Baadhi ya wanachama waliojitokeza kumsindikiza Jaquline Kisanga kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa Nyamagana
 Wanachama wakimpongeza baada ya kuchukua fomu