Header Ads Widget

MTUMISHI WA HALMASHAURI YA MJI TARIME AKANUSHA TAARIFA ZA KUBAKWA NA KULAWITIWA NA MWAJIRI WAKE


Msichana Bahati Ningha aliyeomba radhi kwa kumchafua Mwajiri wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tarime kuwa amembaka na Kumlawiti.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Bw Elias Ntiruhungwa aliyetuhumiwa kumbaka Mwajiriwa wake.

Msichana mwenye umri wa Miaka 19  aliyefahamika kwa majina ya Bahati Niga Mkazi wa Shinyanga ambaye ni mtumishi wa halmashauri ya Mji wa Tarime amekanusha taarifa zilizosambaa katika  mitandao ya Kijamii kuwa amebakwa na kulawitiwa na mwajiri wake ambaye ni Mkurugenzi wa Mji wa Tarime Bw Elias Ntiruhungwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Shinyanga Msichana huyo amesema kuwa kumekuwapo na taarifa nyingi katika mitandao ya Kijamii zikimhusisha yeye kuwa amebakwa na kulawitiwa na Mwajiri wake ambaye ni mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Tarime ambapo amebainisha kuwa jambo hilo siyo la kweli ila  lilifanyika kutokana na shinikizo la baadhi ya watu kwa lengo la kumchafua mkurugenzi huyo.

Bahati amesema kuwa baada ya mtu mmoja aliyekuwa akifanya kazi katika halmashauri hiyo (Mzee Samweli Chomete) aliyekuwa akishirikiana na baadhi ya wanasiasa na wafanyabiashara  kwa utovu wa nidhamu ndipo alipoamua kumtumia yeye kwa kumlaghai kuwa ajitangaze kuwa amebakwa na kulawitiwa na Mwajiri wake kitendo ambacho  kimemfadhahisha na kuidhalilisha familia yake.

“Katika kufanikisha hili waliniondoa nilipokuwa naishi awali na kuhamishiwa kwa mzee Chomete ili kufanikisha ushawishi wao ambapo wanizuia hata kutoka na kufanya mawasiliano ya aiana yoyote”amesema Bahati

Bahati ameongeza kuwa aliahidiwa kiasi cha shilingi milioni 50 toka kwa baadhi ya wanasiasa Mjini Tarime kuwa endapo atafanikiwa kutimiza lengo la kuondolewa kwa Mkurugenzi huyo kwa kashfa ya ngono, atapewa pesa hizo.

  Katika hatua nyingine Bahati amesema kuwa katika maisha yake yote aliyoishi Tarime hajawahi kuwa na mahusiano ya aina yoyote ya kimapenzi na Mwajiri wake kama ilivyoenea mitandaoni.

Amesema kuwa ameamua kuuambia umma ukweli kuwa jambo hilo lilifanyika kwa shinikizo la baadhi ya watu kwa lengo la kumchafua mkurugenzi wa mji Tarime Bw Elias Ntiruhungwa ili aweze kuondolewa katika halmashuari hiyo  kwa njia ya kufukuzwa kazi au  kuhamishwa kutokana na tuhuma za ngono na ubakaji.

Hata hivyo Bahati ameiomba radhi   Serikali na familia ya Mkurugenzi huyo wa Mji Tarime kwa  usumbufu wowote uliyojitokeza kutokana na  habari hizo ziliozenea kwenye miandao ya Kijamii ambapo hakujua ukubwa wa athari zake.

Kwa upande wake Mama Mzazi wa Bahati Bi Amina Kassim  ambaye amezungumza na vyombo vya habari ameeleza kusikitishwa na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijaamii kuwa mwanae amebakwa na kulawitiwa jambo lililowasukuma kufunga safari kuelekea Mjini Tarime kujiridhisha na taarifa hizo ambapo alimkuta mwanae akiwa mzima wa afya huku akisema kuwa tukio na taarifa hizo zilitolewa na watu wasio kuwa na nia njema na maisha ya Mwanae  ambapo ameitaka jamii kutokumwelewa Mtoto wake vibaya.

Bw. Petro Leonard Masato ambaye ni jirani wa familia ya Bw. Niga amesema kuwa baada ya kupata taarifa za Msichana huyo kubakwa na mwajiri wake zilimshitua   kutokana na kuwa karibu na familia hiyo aliwasialana na wazazi wa motto wamrudishe nyumbani na baada ya kurejea alifika akiwa na afya njema tofauti na ilivyoripotiwa awali kwenye mitandao ya kijamii  

Jitihada za kumpata mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Tarime Bw. Elias Ntiruhungwa zimefanyika ambapo amesema kuwa suala la tuhuma za yeye Kubaka na Kulawiti mtumishi   wake amezipata kupitia mitandao ya kijamii na kusema kuwa yeye kama kiongozi wa umma na jamii anapaswa kuwa mfano wa kuigwa hivyo jambo hilo limemsikitisha na kumsononesha sana hapaswi kulielezea zaidi kwa kuwa serikali kupitia vyombo vyake vinavyohusika na uchunguzi vitachunguza suala hilo kwa umakini na kubaini ukweli wa jambo hilo ili haki iweze kutendeka.

Alipotafutwa kwa njia ya simu Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Tarime ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nyamisangura Bw Bashir Abdallah  amekiri kulisikia suala hilo kupitia mitandao ya kijamii na kusema kuwa kwa sasa hawezi kuzungumza zaidi kutokana na vyombo vya dola vinaendelea na uchunguzi wake.

Naye katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Tarime Bw. Hamis Mkaluka amesema kuwa taarifa hiyo waliipokea kwa masikitiko makubwa kuhusu tuhuma za Mkurugenzi Mji Tarime Kubaka na Kulawiti kuhusishwa na tuhuma hizo ambapo amevitaka Vyombo vya ulinzi na Usalama kufuatilia kwa kina suala hilo ili ukweli uweze kubainika  na haki iweze kutendeka.

Mkaluka Ameongeza kuwa  Tarime ni sehemu yenye changamoto nyingi za kisiasa hivyo mambo yanayoendelea yanampa wakati mgumu kubaini jambo hilo iwapo siasa inahusika ndani ambapo ameviachia vyombo vya ulinzi na usalama kufanya yake haraka iwezekanavyo ili kubaini ukweli.

Wiki  Kadhaa ziliyopita zilienea taarifa katika mitandao ya Twitter na Jamii Forum zikimuhusisha  Mtumishi wa halmashauri ya Mji Tarime Bi  Bahati Ningha kuwa amebakwa na kulawitiwa na Mwajiri wake ambaye ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bw Elisa Ntiruhungwa.