Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Nshishinulu, Kata ya Nsalala, Agosti 8, 2026, wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kueleza hatua zilizochukuliwa katika kuboresha huduma za kijamii, ikiwemo kukamilika kwa ujenzi wa Zahanati ya Nshishinulu.
TAZAMA VIDEO👇👇
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Nshishinulu, Kata ya Nsalala, Agosti 8, 2026
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akitembelea Zahanati ya Nshishinulu, Kijiji cha Nshishinulu, Kata ya Nsalala, Agosti 8, 2026, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akitembelea Zahanati ya Nshishinulu, Kijiji cha Nshishinulu, Kata ya Nsalala, Agosti 8, 2026, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akiwa pamoja na wananchi katika Zahanati ya Nshishinulu, Kijiji cha Nshishinulu, Kata ya Nsalala, Agosti 8, 2026, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya zahanati hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Mwamkanga, Kata ya Nsalala, Agosti 8, 2026, wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kueleza hatua zinazochukuliwa katika kuharakisha maendeleo, ikiwemo ujenzi wa Zahanati ya Mwamkanga.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akipiga magoti mbele ya wananchi wa Kijiji cha Mwamkanga, Kata ya Nsalala, Agosti 8, 2026, kuwashukuru kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo hilo, pamoja na kumchagua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Mwamkanga, Kata ya Nsalala, Agosti 8, 2026, wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kueleza hatua zinazochukuliwa katika kuharakisha maendeleo, ikiwemo ujenzi wa Zahanati ya Mwamkanga.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akiwa pamoja na wananchi akitembelea jengo la Zahanati ya Mwamkanga, Kijiji cha Mwamkanga, Kata ya Nsalala, Agosti 8, 2026, kukagua maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo na hatua zilizofikiwa.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akipiga picha ya kumbukumbu na wananchi katika jengo la Zahanati ya Mwamkanga, Kijiji cha Mwamkanga, Kata ya Nsalala, Agosti 8, 2026, baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, akiagana na wananchi wa Kijiji cha Mwamkanga, Kata ya Nsalala, Agosti 8, 2026, baada ya kuhitimisha ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Zahanati ya Mwamkanga.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Said Nassoro, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwamkanga, Kata ya Nsalala, Agosti 8, 2026, wakati wa ziara ya Mbunge Azza Hillal Hamad ya kusikiliza kero za wananchi na kujadili hatua za maendeleo katika kijiji hicho. Picha na Kadama Malunde
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Wananchi wa Vijiji vya Nshishinulu na Mwamkanga Kata ya Nsalala wilayani Shinyanga, wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, kwa kuwaletea maendeleo ndani ya kipindi kifupi cha miezi sita, ikiwamo kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Nshishinulu na kuipaua Zahanati ya Mwamkanga.
TAZAMA VIDEO👇👇
Wametoa shukrani hizo leo Agosti 8, 2026, katika mikutano ya hadhara ya Mbunge huyo ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, alipofanya ziara katika vijiji hivyo kwa nyakati tofauti.
Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Nshishinulu, Kabula Mayaya, amesema wanamshukuru Mbunge huyo kwa kuwaletea maendeleo, na kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho, ambayo kwa sasa ipo katika hatua ya kupakwa rangi.
Naye mwananchi wa Kijiji cha Mwamkanga, Banya Masanja, amemshukuru Mbunge Azza kwa kuipaua zahanati ya kijiji hicho, na kumuomba aendelee kuipambania ili ikamilike na wananchi waanze kupata huduma za afya karibu na maeneo yao.
Anna Ganai
“Tunakushukuru sana Mbunge wetu Azza kwa kutuletea maendeleo ndani ya muda mfupi tu, wewe ndiyo Mbunge sasa, yaani tulikuwa tumechelewa kukupata, lakini sasa tunakwenda kupata zahanati,” ameongeza Anna Ganai.
Naye Diwani wa Nsalala, Shoto Joseph Kulwa, amesema wanamshukuru Mbunge huyo kwa kuwapambania katika kata hiyo, na kuhakikisha wanaanza kupata huduma za afya.
Amesema wananchi wa Kata ya Nsalala. wameishi kwa miaka mingi bila kuwa na zahanati, lakini tangu Azza alipoingia katika nafasi ya ubunge, wameanza kunufaika na juhudi zake za kuwaletea maendeleo.
Mtendaji wa Kata ya Nsalala, Muhindi Mauga, akisoma taarifa ya kata katika mkutano huo, amesema ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Nshishinulu ulianza mwaka 2021 kwa nguvu za wananchi hadi hatua ya renta, lakini Halmashauri pamoja na Mfuko wa Jimbo la Itwangi wamekamilisha ujenzi huo na sasa imefikia hatua ya kupakwa rangi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, amesema Kata hiyo ya Nsalala haikuwa na huduma yoyote ya afya, na kwamba kazi ya Mbunge ni kusemea wananchi wake, na ndani ya miezi sita ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan,amehakikisha Kijiji cha Nshinshinulu kinakuwa na Zahanati, na sasa imekamilika na itakwenda kuwekewa Jiwe la Msingi na Mwenge wa Uhuru Agosti 20,2026.
Ameongeza kuwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, anataka alisema anataka kuhakikisha vifo vya uzazi mama na mtoto zinakwisha kabisa ama kupungua katika taifa hili na kwamba ameshaongea na Mkurugenzi wa Halmashauri watenge fedha za kuleta madawa, pamoja na watumishi na kwamba mwezi Septeba hautaisha Zahanati hiyo itaanza kufanya kazi.
Katika hatua nyingine akizungumza katika kijiji cha Mwamkanga, amesema kupitia fedha za mfuko wa Jimbo walizielekeza kwenye kupaua jengo la Zahanati ya kijiji hicho sh.milioni 15, na kwamba Zahanati ya Nshishinulu ikianza kutoa huduma rasmi, wataelekeza tena nguvu kuikamilisha na Zahanati hiyo.
Amesema pia ndani ya miezi sita, wameweza kutatua changamoto mbalimbali ikiwamo ya ubovu wa miundombinu ya barabara na madaraja, na sasa wanapeleka huduma ya umeme kwa baadhi ya vitongoji, na huduma ya maji.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464
































































