Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Manispaa ya Shinyanga, imepongezwa kuwa kinara wa tuzo ya usafi wa Mazingira kitaifa 2026.
Pongezi hizo zimetolewa jana na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro, wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo.
Amesema, anawapongeza Madiwani na Watumishi wote wa Manispaa ya Shinyanga kwa kuifanya Manispaa hiyo kuwa ya kwanza kitaifa kwa usafi wa mazingira.
“Ni kweli kwamba kuna manispaa nyingi katika taifa letu, lakini unapotafuta manispaa safi kimazingira kuliko manispaa zote, ni Manispaa ya Shinyanga,” amesema Mtatiro.
Aidha, ameitaka Manispaa hiyo kuendelea kuweka mikakati ya kuendelea kuimarisha usafi wa mazingira, ili kuendelea kushika nafasi ya kwanza.
Katika ushindi huo pia mtaa wa miti mirefu Manispaa ya Shinyanga ilishika nafasi ya Tatu kitaifa na kupewa cheti na fedha za kitanzania shilingi milioni nane.
Tuzo hizo zilitolewa Aprili 29, 2026 Wilayani Kibiti mkoani Pwani kwenye maadhimisho ya wiki ya afya kitaifa 2026 na Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa ambapo Manispaa ya Shinyanga ili zawadiwa kombe na fedha za kitanzania Sh. milioni nane.
VIDEO CHINI YA PICHA👇👇
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Salum Kitumbo akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
TAZAMA VIDEO👇👇
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464