Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo akiwa kwenye Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo (katikati), akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (Medication-Assisted Treatment - MAT) lililojengwa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akizungumza wakati akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. 
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 Blog
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeitaka jamii kuacha unyanyapaa dhidi ya waraibu wa dawa za kulevya na badala yake kuwasaidia kupata matibabu, huku ikihimizwa kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya dawa hizo kwa kuwalea vijana katika maadili bora yatakayowalinda dhidi ya kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
Wito huo umetolewa na Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, leo Machi 22, 2026 wakati akifungua Kliniki ya Tiba ya Uraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga akieleza kuwa ni hatua muhimu katika kuimarisha huduma za afya ya umma na kuongeza upatikanaji wa matibabu kwa waraibu wa dawa za kulevya mkoani Shinyanga.
Lyimo amesisitiza kuwa uraibu wa dawa za kulevya ni changamoto kubwa inayogusa afya, uchumi na ustawi wa jamii, na kwamba mapambano dhidi ya tatizo hilo yanahitaji ushirikiano wa wadau wote kuanzia familia hadi ngazi ya Taifa.

Ameeleza kuwa huduma za tiba ya uraibu (MAT) zimekuwa nyenzo muhimu katika kupunguza madhara ya matumizi ya dawa za kulevya kwa kusaidia waraibu kupunguza utegemezi, kudhibiti maambukizi ya magonjwa kama VVU/UKIMWI, pamoja na kupunguza vitendo vya uhalifu na vifo vinavyotokana na matumizi ya dawa hizo.
Amewapongeza wadau waliofanikisha ujenzi huo, likiwemo Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) pamoja na Benki ya CRDB iliyofadhili ujenzi wa Jengo hilo kwa gharama ya shilingi Milioni 145.
Kwa mujibu wa Lyimo, mchango wa Benki ya CRDB unaonesha namna sekta binafsi inavyoweza kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii kwa kuwekeza katika huduma za kijamii zenye manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi.
Ameongeza kuwa uwekezaji huo umeipunguzia Serikali gharama na wakati huohuo kuongeza uwezo wa utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.
Akifafanua zaidi, amesema kliniki hiyo ni ya 22 nchini, hatua inayoonesha dhamira ya Serikali ya kupanua huduma za MAT ili kuwafikia wananchi wengi zaidi wanaohitaji msaada wa matibabu.
Katika kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya, Lyimo amebainisha kuwa Serikali inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ikiwemo kuimarisha udhibiti wa uingizaji na usambazaji wa dawa hizo, kutoa elimu kwa jamii hususan kwa vijana, pamoja na kupanua huduma za tiba, matunzo na utengamao.
Aidha, ametambua mchango wa Tanzania Health Promotion Support kupitia ufadhili wa PEPFAR katika kuendesha kliniki za MAT katika maeneo mbalimbali nchini, akisema juhudi hizo zimechangia kuokoa maisha ya Watanzania wengi.
Lyimo amebainisha kuwa licha ya changamoto ya kupungua kwa baadhi ya misaada ya afya kutoka nje, Serikali imechukua jukumu la kuhakikisha huduma hizo zinaendelea kutolewa bila kukatizwa.
Ameeleza kuwa, baada ya uzinduzi huo, wataalamu kutoka DCEA kwa kushirikiana na Wizara ya Afya wanatarajiwa kutoa mafunzo maalum kwa watumishi wa afya ili kuhakikisha huduma zinaanza kutolewa kwa ufanisi na kwa kuzingatia viwango vya kitaaluma.
Sambamba na hilo, Serikali inaendelea na ujenzi wa kituo cha utengamao cha Taifa katika eneo la Itega jijini Dodoma, kitakachosaidia waraibu kurejea katika jamii wakiwa na uwezo wa kujitegemea.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Health Promotion Support, Dkt. Redempta Mbatia, amesema ujenzi wa kliniki hiyo umetokana na uhitaji mkubwa wa huduma za tiba ya uraibu katika mkoa huo, ambapo hapo awali wagonjwa walilazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo.
Naye Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura, amesema benki hiyo hutenga asilimia moja ya faida yake kwa ajili ya miradi ya kijamii, na kwamba katika mradi huo walitoa shilingi milioni 140 kufanikisha ujenzi wa kliniki hiyo.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, amesema Serikali ya Mkoa imejipanga kuhakikisha upatikanaji wa wataalamu wa afya, vifaa na mazingira rafiki ili kuwezesha utoaji wa huduma bora katika kliniki hiyo.
Huduma za MAT ni mkakati unaotumika kusaidia waraibu wa dawa za kulevya, hususan watumiaji wa opioid kama heroini, kwa kutumia dawa mbadala kama methadone sambamba na ushauri nasaha na ufuatiliaji wa kitabibu.
Nchini Tanzania, huduma hizi zilianzishwa mwaka 2011 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam na zimeendelea kupanuliwa katika hospitali za rufaa za mikoa mbalimbali.
Upanuzi huo umechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza madhara ya matumizi ya dawa za kulevya, ikiwemo maambukizi ya VVU, vitendo vya uhalifu pamoja na athari za kiafya na kijamii kwa waathirika na jamii kwa ujumla.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo (wa pili kushoto), akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026. Wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Yudas Ndungile, wa kwanza kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akifuatiwa na Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia.
Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia (wa pili kulia) akizungumza wakati Uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026. Wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, akifuatiwa na Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, wa kwanza kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kliniki ya MAT iliyojengwa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile akifuatiwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi. Wa kwanza kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Luzila John akifuatiwa na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, pamoja na Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akipata maelezo kuhusu huduma zinazotolewa katika Kliniki ya MAT kutoka kwa mtaalamu wa afya.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo (katikati), akipata maelezo kuhusu Huduma zinazotolewa katika Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo akizungumza wakati akitembelea Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa Jengo la Kliniki ya MAT lililojengwa na Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo akizungumza wakati akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (Medication-Assisted Treatment - MAT) lililojengwa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akizungumza wakati akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akizungumza wakati akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akizungumza wakati akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kamishna wa Kinga na Tiba wa DCEA, Dkt. Peter Patrick Mfisi akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mnufaika wa huduma za MAT, Ibrahim Seif akieleza jinsi alivyofanikiwa kuachana na matumizi ya dawa za kulevya baada ya miaka 10.

Muonekano wa Jengo la Kliniki ya MAT lililojengwa na Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa Jengo la Kliniki ya MAT lililojengwa na Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akisalimiana na Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia.




























