` KATIBU WA UVCCM SHINYANGA MJINI AMEENDELEA NA ZIARA YA KIUTENDAJI KUIMARISHA CHAMA NA JUMUIYA ZAKE

WANDAMAN HOTEL

KATIBU WA UVCCM SHINYANGA MJINI AMEENDELEA NA ZIARA YA KIUTENDAJI KUIMARISHA CHAMA NA JUMUIYA ZAKE

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini imeendelea na ziara ya kiutendaji yenye lengo la kuimarisha chama na jumuiya zake.
Ziara hiyo ilianza jana kwa kutembelea kata za Kolandoto na Chamaguha, huku leo Machi 31, 2026 wamefika katika kata za Kizumbi, Kitangili na Ibinzamata.

Katibu wa UVCCM wilaya hiyo Naibu Katalambula, amesema ziara yao ni ya kiutendaji kwa kukumbushana wajibu na majukumu ya viongozi kwa jumuiya zote, kwa lengo la kuimarisha chama kwa kupeana maelekezo na kuyatekeleza.
Amesema, maendeleo ya nchi bila CCM imara, haiwezi kusongambele, na ili serikali iweze kuwa imara lazima chama kiwe imara, sababu serikali iliyopo madarakani inatokana na CCM, na ndiyo maana UVCCM wanafanya ziara ya kuimarisha uhai wa chama.

“UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini tupo kwenye ziara ya kiutendaji kwa lengo la kuimarisha chama na Jumuiya zake,” amesema Katalambula.
Aidha, ametoa maelekezo kwa viongozi wa mabaraza ya jumuiya hizo, kwamba pamoja na mambo mengine pia wasajili wanachama wapya kuanzia ngazi ya mashina, kuhamasisha ulipaji wa ada za uanachama, na kufanya vikao ya kiutendaji mara kwa mara.

Naye diwani wa Kizumbi Rubeni Kitinya, amepongeza umoja huo, kwa kufanya ziara hiyo, kwamba uchaguzi umekwisha na sasa ni wakati wa kukijenga chama, pamoja na kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.

MAELEZO KATIKA PICHA👇👇
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akizumgumza kwenye kikao cha kiutendaji kuimarisha chama.

Katibu wa Hamasa na Chipukizi Samson Suleiman akizungumza.
Diwani wa Kizumbi Rubeni Kitinya akizungumza.
Diwani wa Kitangili Jonasan Madete akizungumza.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akizumgumza kwenye kikao cha kiutendaji kuimarisha chama.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akizumgumza kwenye kikao cha kiutendaji kuimarisha chama.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464