` UTAMU WA AMANI SOMO KUTOKA KWA WALINDA AMANI WA TANZANIA HUKO SUDAN KUSINI

UTAMU WA AMANI SOMO KUTOKA KWA WALINDA AMANI WA TANZANIA HUKO SUDAN KUSINI

Wakati kukiwa na watu wanaotapatapa kwenye mitandao ya kijamii wakijaribu kuchochea ghasia na uvunjifu wa utulivu, ushuhuda wa askari wa Tanzania wanaorejea kutoka misheni za nje unatoa funzo kubwa kuhusu taabu ya nchi inayopoteza amani. 

Kauli mbalimbali za maafisa na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania waliomaliza muda wao wa kuhudumu katika operesheni ya kulinda amani nchini Sudan Kusini  wamesema Watanzania ni lazima kulinda amani kwani walichoshuhudia huko kinachosha akili.

Walisema hayo wakati wa kuvishwa nishani katika gwaride maalumu, ikiwa ni utambuzi wa mchango wao mkubwa katika kudumisha utulivu chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa.

Tanzania inaendelea kuwa miongoni mwa nchi kinara duniani katika kuchangia askari kwenye operesheni hizi za kimataifa, ikionesha ukomavu wa majeshi yetu na thamani ya amani ambayo nchi yetu imekuwa nayo kwa miongo mingi. 

Askari waliovishwa nishani wamesimulia jinsi walivyokabiliana na changamoto za mazingira magumu na hali ya hatari, lakini waliendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kutoa elimu ya amani kwa jamii ya Sudan Kusini iliyokumbwa na machafuko.

Ujumbe kutoka kwa askari hawa ni wa tahadhari kwa Watanzania wote, hasa vijana, kutokubali kufuata mkumbo wa sauti zinazohamasisha vurugu mitandaoni kwani picha ya nchi inayokosa amani ni ya simanzi na mateso. 

Walinda amani hao wamewashukuru majeshi wenzao kwa ushirikiano walioupata na kutoa wito kwa wananchi wa Sudan Kusini kuendelea kulinda na kudumisha amani ya nchi yao, somo ambalo ni muhimu pia kwa kila Mtanzania anayethamini utulivu uliopo nchini. 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464