` WAHITIMU CHUO CHA BIBLIA PHILADELPHIA WAMETAKIWA KUWA MABALOZI KUTANGAZA NENO LA MUNGU NA KUKEMEA MAOVU KWENYE JAMII

WAHITIMU CHUO CHA BIBLIA PHILADELPHIA WAMETAKIWA KUWA MABALOZI KUTANGAZA NENO LA MUNGU NA KUKEMEA MAOVU KWENYE JAMII



Wahitimu wa ngazi ya Diploma Chuo cha Philadelphia Bible College kilichopo Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga

Mkuu wa chuo cha Calvary Reform Bible Institute Tanzania Lawrence Daffa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya kwanza Philadelphia bible College.

 Na Stella Herman,Shinyanga Press Club Blog

Chuo cha Biblia cha Philadelphia kinachomilikiwa na Kanisa la Philadelphia Miracle Temple Kilichopo Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga kimefanya mahafali yake ya kwanza ya wahitimu wa ngazi ya  Diploma na kuwataka kwenda kuihubiri injili kwa ujasiri.

Akizungumza kwenye mahafali Mgeni rasmi Mkuu wa chuo  cha Calvary Reform Bible Institute Tanzania Lawrence Daffa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya kwanza Philadelphia Bible College amesema elimu waliyopata ikawe chachu ya kuleta mabadiliko.

Amesema wametumwa kwenda kwenye ulimwengu wa vita ya kiroho katika kunyenyua kusudi la mungu na kupinga hila na upotevu wa ufalme wa giza,kwa kuwa dunia ya leo inanjaa ya kiroho na imejaa mkanganyiko wa kimaadili na mara nyingi hupinga ukweli wa neno la mungu.

Amesema ni wakati wa kusimama kwa ujasiri Kupinga hila na upotevu wa ufalme wa giza ambapo amesisitiza kuwa siyo wakati wa kurudi nyuma bali wakati wa kusimama kwa ujasiri.

“Cheti mnachopokea leo si karatasi tu bali ni agizo kutoka mbinguni la kuihubiri injili kwa ujasiri,agizo la kuwasha nuru ya kristo katika giza la dunia hii,agizo la kuishi kwa tofauti kama vyombo vitakatifu na vya haki  mbele za binadamu na mungu”amesema Daffa.

Mkurugenzi wa chuo cha Philadelphia Bible College Askofu Baraka Laizer amesema lengo lao ifikapo mwaka 2030 kwa uwezo wa roho mtakatifu ni pamoja na kuwaendeleza kielimu baadhi ya wahitimu wa Diploma waliohitimu leo ili kupunguza tatizo la upungufu wa walimu.

Wahitimu wakiingia ukumbini
Mkurugenzi wa chuo cha Philadelphia Bible College Askofu Baraka Laizer

Mhitimu ngazi ya Diploma Suzy Luhende Butondo akipokea cheti chake
Wahitimu wa chuo cha Philadelphia wakiingia ukumbini


                  Wageni waalikwa wakishuhudia matukio mbalimbali katika mahafari ya kwanza ya chuo cha Philadelphia 

Sherehe ikiendelea




Zoezi la kupokea vyeti likiendelea George Kulwa akipokea cheti 
Zoezi la kupokea vyeti likiendelea Dionisio Kaijage  akipokea cheti




Mhitimu Suzy Butondo akikata keki 
Mwandishi wa habari wa Jambo FM Eunice Kanumba akimlisha keki Mhitimu wa  ngazi ya Diploma Suzy Butondo


                 Evaline Msangi  ambaye ni mhitimu wa ngazi ya Diploma  akipokea cheti                                  
Wahitimu wakipongezana kwa kulishana keki 

Wahitimu wakifanyiwa maombi maalum na viongozi wa dini ili kuwawezesha kwenda kufanya kazi ya Mungu vizuri.
                                   

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464