Header Ads Widget

JAY NATHWANI ASHINDA MASHINDANO YA GOLF YA ARUSHA OPEN 2022

Jay Nathwani ashinda mashindano ya Golf ya Arusha Open 2022

Mchezaji wa Golf Jay Nathwani wa klabu ya Gymkhana Arusha, ameshinda mashindano ya Golf ya Arusha open 2022 yaliyofanyika uwanja wa Gymkhana jijini Arusha.

Mashindano hayo ambayo yalidhaminiwa na kampuni ya Bima ya Reliance na kishirikisha wachezaji 117.

Nathwani alishinda kwa kupata jumla ya mikwaju 154 na nafasi ya pili ilichukuliwa na aliyekuwa bingwa mtetezi wa mashindano hayo Victor Joseph wa kutoka klabu ya Gmykhana ya jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa mashindano hayo,Prudence Kaijage alimtangaza mshindi kwa upande wa wasichana alikuwa ni Neema Ulomi akifatiwa na Stella Emmanuel.

kaijage alisemakwa upande wa watoto mshindi alikuwa ni Mohamedasad Meloncelli huku katika daraja la A, mshindi alikuwa ni Aliabbas Kermali akifatiwa na Nathaniel Itinda, huku Raju Ladhia akishinda upande wa daraja B akifatiwa na Dismas Seth na daraja C alishinda Dian Vaja akifatiwa na Tinka Sour.

Akizungumza katika hafla ya kutoa zawadi,Mtendaji mkuu kampuni ya ya bima ya Reliance Ravi Shankar aliahidi kampuni hiyo kuendelea kudhamini mashindano hayo kila mwaka ili kukuza mchezo wa golf nchini.

Shankar amesema kampuni hiyo imefarijika kuona idadi ya washiriki hasa wanawake na vijana inaongezeka kutoka mwaka jana ambapo washiriki walikuwa 104 tu.

Mkuu wa idara ya masoko ya kampuni ya bima ya Reliance, Joyce Bendera alisema mwaka huu idadi ya wanawake imeongezeka na kufikia 13 na watoto 24.

"tunapenda kutoa wito kwa wazazi kuendelea kuwapa fursa watoto wao kujitokeza kucheza mchezo huu na Golf kwani ni mzuri"alisema

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi aliyekuwa mgeni rasmi, Mbunge wa jimbo la Arusha mjini, Mrisho Gambo aliwapongeza washiriki wote katika mashindano hayo kwani pia yanachangia kukuza utalii katika jiji la Arusha.

"tunapongeza kampuni ya bima kuendelea kudhamini kwa mwaka wanne sasa mashindano haya ambayo yanakutanisha wachezaji kutoka Afrika ya Mashariki na kwa Arusha ni fursa ya kukuza Utalii na biashara"alisema.

Mwenyekiti wa Gymkhana klabu Julius Karata alipongeza klabu sane ambazo zilishiriki mashindano hayo.

Alizitaja klabu hizo kuwa ni Lugalo na Gymkhana za Dar es Salaam,Gymkhana Arusha,TPC,Moshi Golf ,KiliGolf,Uganda Golf na Klabu ya Kenya

Post a Comment

0 Comments