Header Ads Widget

UKATILI WA KUTISHA MUME AUWA MKE KWA KUMCHOMA KISU SHINGONI

 


Na Shinyanga Press Club Blog 

Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Elia Shija (30) mkazi wa Kijiji cha Didia Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga anashikiliwa na Jeshi la polisi Mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kumchoma kisu shingoni mke wake na kufariki dunia kisha na yeye kujijeruhi kwa kujichoma kisu tumboni. na utumbo wake kutoka nje. 

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 7  nyumbani alipokuwa anaishi marehemu na mumewe,ambapo Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akimtaja marehemu kuwa ni Mariam Julius(26) mkazi wa Kijiji cha Didia huku chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi. 

Alisema mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu mkewe kuwa na uhusiano na wa kimapenzi na mwanaume mwingine ambaye hamjui kwa jina wala sura ndipo aliamuwa kujichukulia sheria mkononi kwa kufanya mauaji. 

Kamanda Magiligimba amesema mtuhumiwa aliwataja baadhi ya watu ambao alidai ndiyo walikuwa wakishirikiana kumtafutia wanaume mke wake ambao ni Lidia Masesa(20) na Mariam Emmanuel (25) wote wakazi wa Kijiji cha Didia. 

Mtuhumiwa wa mauaji hayo amelazwa katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga na hali yake ni mbaya,huku Kamanda akibainisha kuwa taarifa za watu waliokuwa wanadaiwa kumsaidia mke wake kumtafutia wanaume mtuhumiwa alizikuta kwenye maandishi ndani ya daftari lililokuwa chumbani mwao. 

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Shinyanga amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake wafuate sheria na taratibu zilizowekwa ili kupata muafaka. 



Post a Comment

0 Comments