Header Ads Widget

CCM MBOGWE YAZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI YAAHIDI KUTEKELEZA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO


z
Kulia  ni Mgombea ubunge jimbo la Mbogwe (CCM) Nicoedamas Maganga akiwa ameshikiria Ilani ya chama hicho itakayotekelezwa kwa kipindi cha miaka 5 pembeni yake akiwa ni diwani wa kata ya Lulembela, Lyankando Kadushi kwa pamoja wakionesha ilani itakayotumika. 


Salvatory Ntandu- Mbogwe

Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita kimezindua kampeni za Ubunge kwa Jimbo la Mbogwe kwa lengo la kuomba ridhaa kwa wananchi kumchagua mgombea wake Nicodemas Maganga katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza leo na Wananchi wa kata ya Lulembela katika Mkutano wa Kumnadi mgombea  Ubunge wa Jimbo hilo, Mwenyekiti wa (CCM) mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi amewataka wananchi wa jimbo hilo kuwachagua wagombea wa chama hicho katika nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani.

Alisema kuwa CCM Mpya inayoongozwa na Rais wa awamu ya Tano Dk John Pombe Mgufuli imejipanga kuhakikisha inatatua kero za wananchi kupitia ilani yake ya mwaka 2020-2025 ambayo inakwenda kutekelezwa na wagombea wake na kuwataka wananchi kuwa na imani na wagombea  wa chama hicho.

“Mchagueni Rais Dk John Pombe Magufuli, Mchagueni Nicodemas Maganga kuwa mbunge wa jimbo la Mbogwe na wachagueni Madiwani 17 wa kata wa CCM ili wakatekeleza Ilani yetu kwa vitendo, tumedhamiria kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika  sekta za elimu, afya na miundombinu ya barabara,”alisema Kalidushi.

Kwa upande wake Mgombea ubunge wa jimbo hilo, Nicodemas Maganga wakati akiomba kura kwa wananchi amesema kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuongoza jimbo hilo atahakikisha anatatua chagamoto zinazowakabili wananchi hususani katika sekta za afya,elimu,Maji na Miundombinu ya barabara.

“Katika jimbo hili kunachangamoto mbalimbali katika sekta ya afya ikiwemo uhaba wa watumishi wa afya hali ambayo inachangia kuwepo kwa vifo vya  akinamama wajawazito na watoto pindi wanapokwenda kujifungua,”alisema Maganga.

Aliongeza kuwa atahakikisha anaisimamia serikali katika ujenzi wa miundombinu ya barabara ambayo bado ni changamoto katika jimbo hilo ikiwemo Madaraja ili kuwawezesha wananchi kundelea na shughuli za Uzalishaji Mali bila ya kuwa na kikwazo chochote.

Nae Katibu wa CCM wilaya ya Mbogwe amewaomba wananchi wa jimbo la hilo kuhakikisha ifikapo tarehe 28 mwezi wa kumi kuhakakisha wanampigia kura Rais Magufuli,Mbunge  wa jimbo hilo Nicodemas Maganga na Madiwani wote wa chama hicho katika kata zote 17.

Aliongeza kuwa Chama cha Mpinduzi (CCM) kinasera nzuri ambazo zinalenga kuwakomboa wananchi  kwa kuwaboreshea Miundombinu mbalimbali ambapo kwa miaka mitano iliyopita chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli kimetekeleza miradi mikuwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, umeme, Maji, Reli na ununuzi wa ndege ambazo zote zinalenga kuhakikisha watanzania wananufaika nazo.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHAMwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Alhaj Said Kalidushi akisaini kitabu cha Wageni katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni Jimbo la Mbogwe kushoto ni Katibu wa Chama hicho wilaya Mbogwe, Grace Shindika.


Mgombea ubunge jimbo la Mbogwe Nicodemas Maganga akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa CCM waliohudhuria katika ufunguzi wa kampeni za Ubunge wa jimbo hilo.
Mgombea Ubunge Jimbo la Mbogwe Nicodemas Maganga akiwasili katika uwanja wa shule ya msingi Lulembela katika hafla ya uzinduzi wa kampeni za ubunge wa jimbo hilo.
Baadhi ya wagombea Ubunge wa Mkoa wa Geita wakiteta jambo katika mkutano wa ufunguzi wa Kampeni kwa jimbo la Mbogwe.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Geita Alhaj Said Kalidushi akumnadi mgombea Ubunge jimbo la Mbogwe Nicodemas Maganga kwa wananchi.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbogwe kwa kipindi cha 2015-2020 Agostino Masele akimwombea kura Mgombea ubunge wa Jimbo la Mbogwe wa jimbo hilo Nicodemas Maganga.


Baadhi ya Wananchi wanaoliohudhuria katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni wa Jimbo la Mbogwe uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Lulembela.

Mgombea Ubunge wa jimbo la Mbogwe Nicodemas Magaga akielekea kwenda kutoa zawadi kwa vikundi vya ngoma katika hafla ya uzinduzi wa Kampeni katika jimbo la Mbogwe.


Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Agostino Masele akiwashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kumpigia kura katika uchaguzi uliopita kulia ni Katibu wa Siasa na uenezi wa mkoa wa Geita, David Azari.


Vikundi vya sanaa vikitoa burudani