Paroko wa Kanisa Kuu Katoliki Parokia ya Mama mwenye huruma Parokia ya Ngokolo mjini Shinyanga awakutanisha wanandoa 70 kwenye mtoko wa siku ya wapendanao Duniani.

Wanandoa 70 sawa na familia 35 wa Kanisa Kuu Katoliki Parokia ya Mama Mwenye huruma Ngokolo Mjini Shinyanga wamesherehekea siku ya wapendanao duniani kwa kufanya matendo mbalimbali yanayoashiria upendo na uvumilivu kwenye unyumba zao tukio lililoenda sambamba na upandaji wa miti kuashiria Uhai wakiwemo wanadamu.

Wakisherehekea siku ya wapendanao ambayo hufanyika tarehe 14 ya mwezi wa pili kila mwaka wanandoa hao wapata 70 wakiongozwa na paroko wa kanisa kuu parokia ya Mama mwenye huruma Ngokolo Fr. Richard Masunga wamefanya michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa karata, draft pamoja na kucheza nyimbo mbalimbali za asili za makabila yakitanzania ikiwemo ''Iringi'' ya kabila la Wachaga kuashiria upendo na utulivu kwenye ndoa zao matukio yaliyofuatiwa na kula na kunywa.

Wanandoa wakipata Burudani ya miziki yakizamamni (TWIST)
Miongoni mwao waliokuwepo katika mtoko huo ni wanandoa wakongwe waliodumu kwa zaidi ya miaka 45 kwenye ndoa ni Bw.Peter Tesha na Mkewe Imakulata Anthony wamesema siri ya kuishi maisha marefu kwenye ndoa ni kuvumuiliana, kusameheana makosa, kusema asante kwa chochote hata kama ni kidogo na kubwa zaidi ni kumcha mwenyezi Mungu.

Sambamba na hayo wanandoa hao wameshiriki semina ya ndoa wakikumbushwa mambo muhimu namna ya kuimarisha ndoa pamoja na vipaimbele ambavyo ni muhimu kufanyiana bila kukwepa majukumu ya kulea watoto katika njia iwapasayo kwa kuzingati haki na wajibu wao.

Aidha amewataka wanandoa wachanga kuyaishi mafunzo na maelekezo waliyopata wakati wa mafunzo na kujifunza kwa wanandoa wakongwe, kubwa zaidi ni kumcha mwenyezi mungu ili wapate kuwa na maisha marefu ndani ya ndoa zao.






















Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464