SHY WOMEN’S DAY OUT 2025 MAMBO NI MOTO WANAWAKE WATAKIWA KUSHIKAMANA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
SHEREHE ya Wanawake Shy Women’s day Out imefana, huku wanawake wakitakiwa kupendana,kushikamana pamoja na kuchangamkia fursa za kiuchumi na uongozi.
Sherehe hiyo iliyoandaliwa na Kikundi cha Women For Change,imefanyika jana katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga,ambapo mgeni rasmi ni Naibu Spika Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Hassan Juma, huku mshereheshaji akiwa ni Dk.Kumbuka.
Awali akisoma taarifa ya Kikundi cha Women For Change Mwenyekiti wa Kikundi hicho Sara Sawe, amesema kuwa sherehe hiyo ya Women’s Day Out imefikisha miaka Sita sasa,ikiwa na lengo la kuwakutanisha wanawake sehemu moja,kufurahi,kutengeneza mtandao,pamoja na kupeana fursa za kiuchumi.
Amesema kwenye sherehe hiyo hua zinatolewa mada mbalimbali ambazo zinawajengea wanawake maarifa yakiwamo ya kiuchumi,kijamii na kisiasa kutoka kwa watalaamu mbalimbali ambao wamebobea kwenye masuaka hayo.
“Kikundi chetu cha Women For Change tulikianzisha mwaka 2013, kwa lengo la kusaidiana,kuinuana kiuchumi,kushirikia huduma za kijamii pamoja kusidia watu wenye uhitaji,”amesema Sara.
“Baadae ndipo tukaja na wazo la kuwa tunafanya sherehe ya kuwatoa “out” wanawake wa Shinyanga “Shy Women’s Day Out”ili kuwakutanisha pamoja,kufurahi,kubalishana mawazo,kutengeneza “Connection” na kupeana fursa za kiuchumi na sasa sherehe hii imefikisha miaka 6,”ameongeza Sara.
Aidha,amesema kikundi hicho ni mdau mkubwa wa Serikali katika kuchagiza maendeleo, na kwamba wamekuwa wakitoa Madawati shuleni,kusomesha wanafunzi hadi vyuo vikuu,wameshakarabati bweni katika Kituo chakulea watoto wenye Ualbino.
Ametaja misaada mingine ni kuwapatia mitaji Wajasiriamali wadogo na kwamba mipango yao yam waka huu 2025 ni kufanya pia ukarabati wa Jengo la Magereza ya Shinyanga kwa ajili ya wafungwa kulitumia kwa chakula na kazi hiyo walishaianza na imefikia asilimia 85.
Amesema mipango mingine ni kuwa na Taasisi kubwa ya kifedha kwa ajili ya kusaidia wanawake,pia kujenga ukumbi mkubwa na hata kutumika kwa mikutano ya kitaifa.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi,akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha kwenye sherehe hiyo, amekipongeza kikundi hicho cha Women For Change kwa kuwakutanisha wanawake wenzao na kupeana maarifa mbalimbali.
Mgeni rasmi Naibu Spika Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Hassan Juma, amewashukuru Women For Change kwa kumheshimisha, huku akiwasihi wanawake waishi kwa kupendana,kushikamana ili wapate kunyanyuka kwa pamoja.
Amesema matatizo ya wanawake karibia yote yanafanana hivyo kupitia sherehe hiyo,kila mmoja abadilike sasa na kuishi kama ndugu,kushikana mikono na kuinuana kiuchumi.
Amewataka pia wanawake watumie fursa zilizopo za kiuchumi na kwamba sheria inawapatia wanawake kipaumbele katika kupata Zabuni,pamoja na kuchangamkia mikopo ya halmashauri asilimia 10.
Katika hatua nyingeni amewataka wanawake wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi mkuu 2025 kwa nafasi ya Udiwani na Ubunge, sababu nafasi ya Rais yupo Dk.Samia kwa upande wa Tanzania na Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi.
Pia,amewataka wananchi katika kuelekea kwenye uchaguzi huo waendelee kudumisha amani na Utulivu, pamoja na kuendelea kuuenzi Muungano.
TAZAMA PICHA👇👇
Naibu Spika Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Hassan Juma akizungumza.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi akizungumza.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Women For Change Sara Sawe akizungumza.
Mwenyekiti wa Sherehe ya Women's Day Out 2025 Faustina Kivambe akizungumza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza.
MC Dk.Kumbuka akisherehesha.
Naibu Spika Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mgeni Hassan Juma (kulia)akiwa na Mwenyekiti wa Women For Change Sara Sawe.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi (kushoto)akiwa na Mwenyekiti wa Sherehe ya Women's Day Out Faustina Kivambe.
Mr Black akitoa somo la uchumi.
Sherehe ya Women's Day Out ikiendelea.
Utoaji wa vyeti vya shukrani kwa wadhamini wa sherehe hiyo ukiendelea.
Picha za pamoja zikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464