Mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Kisena Mabuba
Na Kareny Masasy,
PROGRAMU jumuishi ya Taifa ya Makuzi na Malezi na Maendeleo ya Awali ya mtoto ( PJT-MMMAM ) ina lengo la kushughulikia mahitaji mahsusi yaliyotambuliwa baada ya kufanya uchambuzi wa hali halisi ya huduma za program hiyo kwa watoto wenye umri miaka 0 hadi minane (8).
Katika utambulisho wa programu ya PJT-MMMAM iliyozinduliwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambapo viongozi na wataalamu wa sekta mbalimbali walihudhuria.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kisena Mabuba akiwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo anakasirishwa na baadhi ya wazazi kuwaachia watoto kwenda kwenye vibanda vya video nyakati za usiku wakati wakuangalia mechi za mpira.
Mabuba anatoa ushuhuda anasema katika kibanda kimoja majira ya saa tano usiku hivi karibuni aliwakuta watoto wenye umri wa miaka sita wawili wakiwa wamechangamana na wakubwa wakiangalia mechi za mpira zinazoendelea.
“Nilichukua jukumu la kuwakemea watoto hao nakutaka kufahamu wazazi wao lakini nilikwenda moja kwa moja kwa mhusika wa kibanda hicho nakumueleza kuhusu watoto hao nikapiga marufuku watoto nyakati za usiku”anasema Mabuba.
Mabuba anasema suala la Malezi na Makuzi linamafundisho yake kwa madhehebu ya dini kuna madrasa na sunday school na kila taasisi inatengeneza kupata misingi ya watoto waliokuwa kwenye hali ya utimilifu wa ukuaji na kimaadili.
Mabuba anasema Siku hizi jamii ilivyo sio kama zamani kwani imekuwa ikiona watoto ambao hawakuwazaa haina haja ya kuwaangalia bali ni mzazi mwenyewe aliyezaa ndiyo jukumu lake.
“Msingi wa mradi huu ni kufichua uovu na kutoa elimu katika jamii na viongozi wa dini tusimame pamoja tunaweza kuwaokoa watoto kupitia Programu ya PJT-MMMAM hii itunyanyue na itubadilishe kifikra”anasema Mabuba..
Mabuba anasema Taifa limeanza kuchukua misingi ya malezi kwa watoto wote kwani linaapozungumziwa sula la malezi na makuzi ni jambo kubwa kwa taifa haiwezekani kuzingatia suala la malezi bora bila kusema lishe,afya,elimu , ulinzi na usalama.
Mwezeshaji ambaye ni mratibu wa afya ya uzazi ya mama, baba na mtoto kutoka mkoani Shinyanga Halima Hamis anasema programu imekuja mahsusi kwa kuanzia umri o hadi miaka nane.
Hamis anasema Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto yanaanzia tangu mtoto akiwa tumboni anazaliwa tayari ubongo wake unakuwa ukitambua nakuzaliwa akiwa anajua hivyo wasipowekeza vizuri kwa watoto wanaweza kutengeneza taifa lisilokuwa na watu timilifu.
“kwa mujibu
wa takwimu ya taifa ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 imeeleza watoto wenye umri wa kuanzia
o hadi miaka nane ni zaidi
ya watoto takribani 16,000 hapa nchini ambapo ni sawa na asilimia 30 ya watanzania wote hivyo kundi hili ni muhimu"anasema Hamis.
Hamisi anasema yapo mambo mengi yanayopelekea kuwaathiri watoto kwani suala la malezi na makuzi ya watoto lazima ziangaliwe nguzo tano ambazo ni Afya,Lishe,Malezi yenye mwitikio,Elimu au ujifunzaji wa awali ikiwemo ulinzi na Usalama.
"Kuna mambo mengi yanatokea kuathiri ukuaji wa watoto kwani mtoto akifanyiwa ukatili au kudhalilishwa kitendo hicho kitaamuathiri hadi ukubwani nakushindwa kufanya majukumu yake kikamilifu”anasema Hamis.
.“Serikali imeona ipo changamoto kwenye jamii kwa kufuata Mila na destruri zilizo mbaya kwani zipo nzuri ambazo zinaweza kufuatwa ili kuweza kuwafikisha watoto katika ukuaji ulio timilifu”anasema Halima.
Ofisa ustawi wa jamii kutoka mkoani Shinyanga Lyidia Kwesigabo anasema programu hii itakuwa endelevu inapaswa kuanza kutekelezwa kwenye kila sekta ambazo zimegusa watoto hawa kwa kubuni mikakati.
“Tukiangalia suala la elimu, afyalishe,Malezi yenye mwitikio na ulinzi na usalama yote yanatuhusu tukishikamana kwa pamoja hakuna mtoto yoyote atakaye achwa nyuma na hili alilosema mkurugezi kuhusu watoto tuwalinde sote jamii nzima”anasema Kwesigabo.
Mchungaji wa kanisa la Angilikana lililopo kata ya Iselamagazi Fanuel Shemtoi anasema yaliyoelezwa na mwezeshaji kupitia program ya PJT-MMMAM yamemgusa nakusema alikuwa hafahamu ndiyo kwanza amepata darasa upya.
Shemtoi anasema alichogundua bado jamii inaendekeza mila na desturi katika malezi ya watoto wakifuata mgawanyiko wa majukumu katika familia ambapo baba amejikita kwenye utafutaji na ikifika jioni ndio kwenda kwenye vibanda vya mpira hawakai na watoto wao kuwapa malezi yenye mwitikio.
“Suala la ulinzi na usalama wa mtoto linaachwa kwa mama pekee lakini hali hiyo imetokana na jamii yenyewe kukosa elimu hii mapema hata kupitia kanisani sasa tutaanza kutoa mahubiri kwa waumini wetu”anasema Shemtoi.
Diwani wa kata ya Iselamagazi Isack Sengerema anasema watoto wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili na watu wazima kuna tukio moja lilitokea hivi karibuni la watoto kulawitiwa hivyo kupitia program hii jamii ikiielewa vizuri watoto watakuwa salama zaidi.
Baadhi ya wazazi wa kata ya Iselamagazi Musa Shija na Zawadi Moza walipohojiwa na mwandishi kuwaruhusu watoto nyakati za usiku kwenda kwenye vibanda vya video wanasema ingawa wamekuwa wakiwafuata watu wazima ni makosa naona wanaingia nao kwa kificho.
Wataalamu na baadhi ya viongozi wa kwenye jamii wakiwa kwenye uzinduzi wa PJT-MMMAM
Wataalamu mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Kisena Mabuba.
Afisa ustawi wa Jamii kutoka mkoani Shinyanga Lyidia Kwesigabo akitoa maelekezo katika kikao cha PJT-MMMAM
Wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Wataalamu wakisikiliza maelezo kutoka kwa mkurugenzi.
0 Comments