Header Ads Widget

WANANCHI WA KIJIJI CHA NHOBOLA WATOA KILIO CHAO KWA MBUNGE KUNYANYASWA NA SUNGUSUNGU

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniface Butondo akizungumza na wananchi wa kata ya Talaga halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga

Suzy Luhende Shinyanga press blog

Wananchi wa kijiji cha Nhobola kata yaTalaga halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wametoa kilio chao mbele ya mbunge wa jimbo hilo Boniface Butondo cha kunyanyaswa na jeshi la jadi la sungu sungu la kijiji hicho kwa kuwatoza Sh 300,000 hadi sh 1 milioni pale wanapokutwa na ugonvi wa kifamilia au kusingiziwa wanamakosa, hali ambayo imekuwa ikisababisha ndoa nyingi kuvunjika na watoto kupata shida na kukimbilia mitaani.

Hayo wameyasema leo wakati wakitoa kilio chao mbele ya Mbunge wa jimbo hilo, wakati akiwa kwenye ziara yake ya kusikiliza kero mbalimbali katika jimbo lake, ambapo wamesema wamechoka kunyanyaswa kwa kupigwa faini kuanzia Sh 300,000 hadi Sh 1 milioni na wasipotoa wanatengwa na jamii.

Baadhi ya wananchi hao akiwemo Juliana Bilu wamesema sungusungu wamekuwa vinara wa rushwa katika kijiji hicho, kwani wamekuwa watu wakutegeshea ugomvi kwenye familia na kukimbilia kutoza faini kubwa, kuku ikiibiwa anasingiziwa mtu ambaye anaonekana anauwezo wa kutoa fedha anapigwa faini bila kusikilizwa.

"Kwa nini sungu sungu wanatufanya hivi tumechoka kukaa kwenye hali ya kunyanyaswa na sungu sungu, hali hii itasababisha watu waanze kukatana mapanga kwa hasira walizonazo,tunakushukuru sana kwa kuja tunakuomba utusaidie mbunge wetu hawa watu ni wakatili sana na wamekuwa ni kero kubwa hapa kijijini," amesema Bilu.

Lupande Salala amemuomba mbunge awasaidie waondokane na kilio hicho ambacho kimekuwa cha muda mrefu sasa, kwani sungu sungu hao wamekuwa wakitoza faini hizo na wala hawawasomei wananchi taarifa ya mapato na matumizi.

"Tunashangaa hawa sungusungu wanatutoza faini, lakini hata hawatusomei mapato na matumizi,mwezi wa tano walisoma lakini ilikuwa ni feki haina mchanganuo hawafanyi kazi hawalimi wametufanya sisi ndiyo mashamba yao sasa tumechoka tunakuomba mheshimiwa mbunge utusaidie,"amesema Salala.

"Ukatili wa kijinsia haupo kwa sasa ila sungusungu ndio inatufanyia ukatili sasa huu ni usumbufu wa maisha, tumekuwa tukiteseka sisi lisipofanyiwa kazi hili tutamalizana kukatana mapanga, huu ni usumbufu wa maisha tunaonewa sana, hivyo lifanyiwe kazi kwa haraka amesema, Salala.

Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Richard Dominiko amesema tatizokubwa lililopo kijijini hapa wamekuwa wakiwapigia kura wao wenyewe hawa viongozi wa sungusungu kwa sasa watakuwa wamejifunza hivyo alimuomba mwenyekiti aitishe mkutano ili iweze kuundwa sungusungu nyingine ambayo itaanza upya.

"Na niombe msiwahukumu wote wengine wapo wazuri, lakini wengine wanaweza kuendelea, kwani kuna wengine hawashirikishwi ndiyo maana kuna baadhi yao wanafikia wakati wanajiuzulu sababu hawashirikishwi chochote,"amesema Dominiko.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo hilo Boniface Butondo amemuomba diwani wa kata hiyo kusimamia suala hilo, ili wananchi waondokane na kero ya sungusungu kwani wananchi wanalia kwamba wamekuwa mashamba ya sungusungu hii haikubariki wananchi kuendelea kuishi bila amani na kwa kutoa faini zisizokuwa na utaratibu kila kitu kinautaratibu wake.

"Simamia hawa watu kwani wanalia wamekuwa mashamba ya watu, na sungusungu ni marufuku kutoa faini zisizokuwa na utaratibu nitamuagiza OCD atakuja ndani ya wiki hii akutane na nyinyi na nitamtaka awape elimu afanye mkutano wa ndani na wa nje, haiwezekani watu wanapigwa faini Sh 1. milioni na vikao kufanyiwa vilabuni hii haikubaliki hata siku moja,sungusungu tunawajua ni wa muhimu wanalinda na kusaidia jeshi la polisi, kwa sababu polisi hawawezi kulinda kila kijiji,"amesema Butondo

"Kweli kesi za ajabu ajabu tu mtu kagombana kifamilia,watu wanabishana wanatozwa faini kuanzia laki tatu, hapa watu wengine wamevunja ndoa baada ya ya wenza wao kuuza mali za nyumbani ili wasitengwe walipe faini walizoambiwa,lakini pia nitawaomba polisi kutoa elimu kwa sungusungu wajue ukomo wao na kazi za sungu sungu,pia askari polisi aliyepangiwa katika kata hii aje akae karibu na wananchi kuliko kukaa wilayani huku migogoro kama hii ikikosamtu wakuitatua,"amesema Butondo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nhobola Kabangala Lubarigi amesema kutokana na kilio cha wananchi anaenda kuivunja kamati ya sungusungu na kufanya uchaguzi siku ya ijumaa na kufanya uchaguzi wa viongozi wa sungusungu ili wachaguliwe wengine.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniface Butondo akizungumza na wananchi wa kata ya Talaga halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniface Butondo akizungumza na wananchi wa kata ya Talaga halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniface Butondo akizungumza na wananchi wa kata ya Talaga halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniface Butondo akizungumza na wananchi wa kata ya Talaga halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniface Butondo akizungumza na wananchi wa kata ya Talaga halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniface Butondo akizungumza na wananchi wa kata ya Talaga halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Wananchi wa kata ya Talaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga wakimsikiliza mbunge wa jimbo hilo Mbunge wa Jimbo hilo Boniface Butondo akizungumza baada ya wao kutoa kero zao mbalimbali

Mwenyekiti wa kijiji cha Nhobola Kabangala Lubarigi akifafanua jambo kwenye kikao cha mbunge

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu akizungumza kwenye kikao hicho
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Nhobola kata ya Talaga akitoa kero yake ya kunyanyaswa na Sungusungu

Mwananchi wa kijiji cha Nhobola skitoa kero yake mbele ya mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo
Mwananchi wa kijiji cha Nhobola skitoa kero yake mbele ya mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo

Juliana Bilu akitoa kero yake mbele ya mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo

Diwani wa kata ya Talaga Richard Dominiko akifafanua jambo kwenye kikao cha mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo
Diwani wa kata ya Talaga Richard Dominiko akifafanua jambo kwenye kikao cha mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo

Post a Comment

1 Comments