Header Ads Widget

BWAWA LA MGODI WA ALMASI MWADUI WILAYANI KISHAPU LABOMOKA NA KULETA ATHARI KWA WANANCHI

Muonekano wa Tope likiendelea kusambaa kwenye makazi ya watu, mara baada ya bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui kubomoka na kusababisha athari kwa wananchi.

Na Marco Maduhu, KISHAPU

Bwawa la Mgodi wa Almasi Mwadui wilayani Kishapu, limepasuka na kutiririsha tope kwenye makazi ya watu na kusababisha mashamba kufunikwa, huku wananchi wakikimbia makazi yao.

Imeelezwa kuwa bwawa hilo limepasuka leo majira ya saa 4 asubuhi na kuanza kutiririsha tope zito na kuharibu makazi ya watu pamoja na mashamba yao.

Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Ng’wang’olo Kaya ya Mwadui Luhumbo Tabu Kikuya, akizungumza na waandishi wa habari ambao wamefika eneo la tukio, amesema baadhi ya nyumba za wananchi zimefunikwa na tope na wamekimbia Kaya zao huku mashamba na visima vya maji vikifunikwa.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amesema kwenye tukio hilo hakuna vifo ambavyo vimetokea, zaidi ya Kaya na mashamba kuathirika, na tayari wananchi wameshapewa msaada wa chakula na maji, wakati Serikali ikiendelea na taratibu zingine.

Post a Comment

0 Comments