Header Ads Widget

MADIWANI KISHAPU WAPITISHA BAJETI YA ZAIDI YA SH BILLIONI 44.9

 

 Kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Kishapu kilijadili kupitisharasimu ya bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 kiasi  cha zaidi y ash Billioni 44.9

 

Katibu wa chama cha Mapinduzi  wilaya ya Kishapu Peter  Mashenji akisisitiza ukusanyaji wa mapato kwa madiwani wa halmashauri hiyo.

 

Na Kareny Masasy,

MADIWANI wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu imepitisha  rasimu ya bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 kiasi  cha zaidi y ash Billioni 44.9 huku  wakisisitiza kushirikiana katika ukusanyaji wa mapato ya ndani kupitia vyanzo vipya walivyoviibua.

Kabla ya kuipitisha bajeti hiyo jana katika kikao maalum cha baraza la madiwani  ambacho kilikuwa na ajenda ya kupitisha rasmi ya mapendekezo ya bajeti mkurugenzi wa halmashauri hiyo Emanuel Jonson amesema kuwa  katika bajeti hiyo  ukusanyaji wa mapato ya ndani ni sh Billioni 4,matumizi ya kawaida shBillioni moja na miradi ya maendeleo ni sh Bilioni 16.

“Ushirikiano unatakiwa na taarifa za ukusanyaji ziwe ajenda kwa  watendaji wa vijiji na kata  katika vikao vyao  na kueleza vyanzo vipya walivyoviibua  ambapo nina ahidi  bajeti hiyo itakwenda kama ilivyopangwa”amesema  Jonson.

 Mwenyekiti wa halmashauri hiyo William Jijimya amesema kuwa mpango wa bajeti wa  zaidi ya sh Billioni 44.9  hii ni dira  ya Kishapu   wamepitisha  bajeti hiyo  na kutaka kuibua vyanzo vipya vya ukusanyaji mapato  na kuelekeza kwenye matumizi ili kuondoa changamoto kwa wananchi  na kuhakikisha fedha hizo kuzipata kwa asilimia 100.

Baadhi ya madiwani hao  akiwemo diwani viti maalum  Felister  Yahula na Bushi Mpina kutoka kata ya Mwamalasa  wamepongeza bajeti hiyo  na kudai ni nzuri  kwani wamepitisha kwa nguvu zote na wako tayari kushirikiana kwani kuna vyanzo vingi vya mapato.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amesema kuwa  kamati ya fedha ndiyo inatakiwa kusisitiza ukusanyaji wa mapato na kusimamia matumizi yake  na siyo bajeti ilivyopangwa  kuivuruga na kuitumia kwenye masuala ya dharura .




Kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya  wilaya ya Kishapu  wakisikiliza kwa makini  

 Diwani wa kata ya Songwa Abdul Ngoromole akiongea kwenye kikao cha baraza la madiwani.

Post a Comment

0 Comments