Header Ads Widget

SERIKALI YAIPONGEZA CRDB, YAELEZA MKAKATI KUPUNGUZA FOLENI TAASISI ZA UMMA


Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Faustine Ndungulile (wapili kulia)akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kuhusu huduma za CRDB Wakala kupitia Shirika la Posta. Wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Clarence Ichwekeleza.
 

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Serikali imepongeza mashirikiano ya Ubia yaliyoingiwa kati ya Shirika la Posta Tanzania na Benki ya CRDB huku ikibainisha kupitia Mpango wa Tatu wa Maendeleo ya Miaka Mitano imejipanga kuhakikisha wananchi  wanapata huduma za kifedha kwa njia za mifumo ya kidijitali ili kupuguza msongamano  katika ofisi  za taaasisi za umma na binafsi nchi nzima

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari , Dkt. Faustine Ndungulile katika Uzinduzi wa Huduma za CRDB Wakala Katika Ofisi za Shirika hilo.

Amesema takwimu za Ripoti ya Ujumuishi wa Fedha ya Finscope  inaonyesha asilimia  16.7 ya Watanzania wote wanatumia  huduma za benki kidijitali, huku asilimia 28 hawana huduma za kidijitali hivyo asilimia 35 ya watu wanatakiwa kurasimishwa katika mifumo ya kidijitali.

"Nawapongezeni Posta na CRDB kwa ushirikiano wenu  mnaonyesha wazi mmepania kuendelea kupanua wigo wa utoaji huduma kwa pamoja  nawaomba mjitahidi muwafikie Watanzania wote," amesema Dkt. Ndungulile.

Amebainisha kuwa tayari Serikali imeshaanza kufanyia kazi mifumo hiyo katika mikoa ya Dar es Salaamn na Dodoma lengo likiwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma  za malipo bima ya afya, pensheni, malipo ya bili za maji, umeme, pamoja na malipo ya usajili wa kampuni kwa njia za kidijitali.

Amesisitiza kuwa Serikali imeshatenga Sh Bilioni 300 kwa ajili ya Mradi wa Tnzania ya Kidijitali na kwamba kupitia Mradi wa Anuani ya Makazi na Postikodi itahakikisha kila eneo lina namba mizigo na vifurushi inafika kwa wakati maeneo husika.

Ametoa rai kwa Mameneja wa Mikoa wa shirika hilo kuutumia viizuri ushirikiano kwa kufanya kazi kwa ufanisi pamoja na kutoa huduma bora kwa wateja kwani kutasaidia kuongeza idadi ya watu wanaotumia za CRDB na Posta kwa mifumo ya kdijitali.

Kwa upande wake Kaimu Postamata Mkuu, Macrice Mbodo amesema shirika hilo limefaidika na wizara hiyo kwani huduma za Serikali ikiwemo leseni y audereva, biashara na vyeti vitolewa na posta, serikali kuanzisha duka la mtandao ambapo ununuzi na uuzaji wa bidhaa hufanyika kupita mtandao pamoja utoaji wa huduma za posta kupita simu za mikononi..

Naye Mkuurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela amesema CRDB itafungua matawi  zaidi 200 na kwamba ilianza na mawakala 200 kwa sasa ina zaidi 20,000 huku akisisitiza mawakala wapya  watapewa elimu wawe na weledi kutoa huduma bora.

Nsekela amesema CRDB imeamua kuwekeza katika teknolojia ya kidijitali ili kuweza kuwarahishia na kuwafikia wateja wao nchi nzima pamoja kuongeza watu wanaotumia mifumo ya kidijitali.

Mkuu wa Kitengo cha Uwakala na Usambazaji wa benki hiyo, Erick Wille amesema kupitia ushirikiano huo pande zote mbili zitaongeza ufanisi  pamoja na kuongeza ajira 250 nchi nzima.

Erick amefafanua huduma zitakazopatikana ni ufunguzi wa akaunti, namba za NIDA, Huduma za kutoa na kuweka pesa, malipo ya ada, tozo za Serkali za taasisi zaidi ya 200, manunuzi, bima pamoja na malipo ya bili z umeme na maji.

Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara wa Shirika la Posta Constantine Kasese amesema shirika hilo lina Ofisi 67,000 duniani kote huku likiwekeza katika majengo 167 ya biashara na makazi.

 

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Faustine Ndungulile (katikati) akikata utepe kuzindua huduma za CRDB Wakala kupitia Shirika la Posta. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wapili kushoto), Kaimu Postamasta Mkuu, Macrice Mbodo (wapili kulia) na Mkurugenzi wa Mawasiliano Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Clarence Ichwekeleza (wakwanza kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya CRDB, Toyi Ruvumbangu (wakwanza kushoto).

 

Post a Comment

0 Comments